CURRENT NEWS

Thursday, October 13, 2016

UMOJA WA MADEREVA MLANDIZI WACHANGIA UJENZI WA MAKAZI YA POLISI


Mkuu wa kituo cha polisi cha mlandizi mrakibu Silvester Njau ,akiwa amebeba mfuko wa saruji na mwenyekiti wa umoja wa madereva wa Mlandizi-Dar es salaam ,Richard Milinga kutoka katika gari iliyokuwa imebeba mifuko hiyo waliyotoa msaada madereva hao kusaidia ujenzi wa makazi ya polisi MlandiziKatibu wa chama cha mapinduzi (CCM)Kibaha Vijijini Enerst Makunga ,akizungumza na waandishi wa habari jinsi wanavyoshiriki bega kwa bega kuhamasisha kukamilisha ujenzi wa makazi ya polisi Mlandizi

Mwenyekiti wa umoja wa madereva mlandizi-Dara es salaam Richard Milinga akipeana mkono na mkuu wa kituo cha polisi Mlanzidi ,mrakibu Sivester Njau mara baada ya umoja huo kukabidhi matofali na mifuko ya saruji ili kusaidia ujenzi wa nyumba mbili kubwa za polisi.

Mkuu wa kituo cha polisi Mlandizi Mrakibu Silvester Njau,akizungumza na baadhi ya madereva wa mlandizi-Dar es salaam na waandishi wa habari kuhusiana na ujenzi wa makazi ya polisi unaoendelea.

Cap:Umoja wa madereva Mlandizi-Dar es salaam wakishiriki nguvu kazi katika ujenzi wa makazi ya nyumba mbili za polisi zinazojengwa nyuma ya kituo cha polisi cha Mlandizi,ili kupunguza adha ya kuishi uraiani kwa polisi hao(Picha na Mwamvua Mwinyi)


Pic:0010


Pic:0009
Cap:

Pic:0008
cap:(picha na Mwamvua Mwinyi)

Pic:0007
cap:(Picha na Mwamvua Mwinyi)

Pic:0004
cap:(Picha na Mwamvua Mwinyi).

Na Mwamvua Mwinyi,Kibaha
ASKARI polisi katika kituo cha polisi Mlandizi,Kibaha Vijijini mkoani Pwani,wanakabiliwa na changamoto ya kuishi uraiani kwenye nyumba za kupanga kutokana na ukosefu wa makazi kwa ajili yao.
Ukosefu wa nyumba za polisi hao husababisha kuchelewa kutekeleza majukumu yao ya kazi na kuwapa usumbufu hasa kukitokea dharura nyakati za usiku.


Mkuu wa kituo cha polisi Mlandizi,mrakibu Silvester Njau alieleza tatizo hilo,wakati alipokuwa akipokea msaada wa mifuko ya saruji na matofali kutoka katika umoja wa madereva wa Mlandizi-Dar es salaam ili kusaidia ujenzi ulioanzishwa wa nyumba mbili za polisi.
Alisema changamoto hiyo ni kubwa ambayo imemsukuma kuanzisha ujenzi huo ambapo utakapokamilika utawezesha kuishi familia tatu hadi sita .
“Kwasasa askari wote tunaishi uraia ambako ni mbali ikiwemo Chalinze,Kibaha,Mbezi,Kiluvya ,Kibamba hivyo kutuweka katika wakati mgumu na mazingira ya kazi”

“Ukimwita askari may be usiku inakuwa ni ngumu sana kufika ukizingatia usafiri wa public nyakati za usiku mwingi unakua haupo hivyo ni changamoto kubwa”alisema mrakibu Njau.

Alieleza kuwa wanaanza na ujenzi wa nyumba hizo mbili na baadae wataendelea na zoezi hilo ili kuhakikisha kero ya kukosa makazi ya karibu unabaki historia.

Mrakibu Njau ,alisema kila mmoja anajukumu la kulinda nchi hivyo anaomba wadau wa amani wajitokeze kuchangia kwa ari na mali ili kuondokana na kero ya ukosefu wa nyumba kwa askari.

Alikishukuru chama cha mapinduzi (CCM)Kibaha Vijijini kwa ushirikiano wake wa kuhamasisha wadau na makundi mbalimbali ambapo wameweza kuzungumza na umoja wa madereva ambao wamejitokeza kusaidia.
Akikabidhi msaada huo,mwenyekiti wa madereva wa Mlandizi-Dar es salaam,Richard Milinga,alisema wanatambua umuhimu wa polisi na amani hivyo wameguswa kuchangia mifuko 10 ya saruji na matofali 400 vyenye thamani ya sh.250,000.
Alisema wanaendelea kujichangisha na baadae wanatarajia kutoa mifuko mingine 25 ya saruji ili kupunguza kero hiyo inayowakabili askari.

Awali katibu wa CCM ,Kibaha Vijijini ,Enerst Makunga ,alisema mrakibu huyo aliwaeleza juu ya kuanza kwa ujenzi huo na kutokana na umuhimu wa jambo hilo wameamua kuhamasisha wadau wa maendeleo.

Alisema makazi  hayo yatakapokamilika polisi watafanya kazi kwa tija kulinda jamii,usalama na amani iliyopo.
Makunga alisema umoja wa madereva Mlandizi wamechangia kwa moyo sio kama wana hela nyingi hivyo ni jukumu la makundi na watu wengine kuunga mkono jambo hilo.
‘Wafanyabiashara ,viongozi na mti yeyote anaeguswa ajitokeze, 
kwa kutambua huwezi kufanya kazi ama kufanyabiashara zako kama huna amani na ulinzi wa uhakika”alisema Makunga.

Alieleza chama cha mapinduzi kitaendelea kuwa bega kwa bega na jeshi la polisi kwa lengo la kuhakikisha sekta ya ulinzi na usalama inaimarika na hatimae kupambana na uhalifu Mlandizi na kulinda usalama wa watu na mali zake.


Mwisho
 
Copyright © 2014 Mkono Wangu Production Designed by EvMak Tanzania