CURRENT NEWS

Tuesday, October 25, 2016

WANAMGAMBO WASHAMBULIA MANDERA, KENYA

Watu kadha wanahofiwa kufariki baada ya watu wenye silaha kushambulia eneo moja la makazi mjini Mandera, kaskazini mashariki mwa Kenya.
Polisi na wanajeshi kwa sasa wanafanya msako na kushika doria mjini.
Taarifa zinasema milipuko mitano ilisikika kabla ya ufyatulianaji wa risasi kutokea.
Eneo lililoshambuliwa huishi sana watu kutoka nje ya mji huo.
Maafisa wa polisi wameambia BBC kwamba watu wanne wameuawa na wengine wanne kujeruhiwa.
Mji wa Mandera umekuwa ukishambuliwa mara kwa mara na wanamgambo wa al-Shabaab, kundi linalopigana dhidi ya serikali inayoungwa mkono na Umoja wa Mataifa katika taifa jirani la Somalia.bbc
 
Copyright © 2014 Mkono Wangu Production Designed by EvMak Tanzania