CURRENT NEWS

Tuesday, November 29, 2016

ASKARI POLISI AFA BAADA YA KUJIPIGA RISASI KIBAHA


Na Mwamvua Mwinyi,Kibaha
ASKARI mwenye namba H.3348 PC Armand Evarist Furaha 33B,amejipiga risasi bila kukusudia na kusababisha kifo chake huko wilayani Kibaha, mkoani Pwani,wakati akielekea kwenye lindo kwa mkuu wa wilaya hiyo.
Kaimu kamanda wa polisi mkoani hapo, SSP Blasius Chatanda,aliyasema hayo kwa waandishi wa habari wakati alipokuwa akitolea ufafanuzi tukio hilo.
Alieleza kuwa novemba  28 majira ya saa moja usiku, maeneo ya Mailmoja eneo la sokoni kata ya Mailmoja ,askari huyo alijipiga risasi kwa bahati mbaya ambapo alifariki dunia wakati akipatiwa matibabu katika hospitali ya rufaa ya Tumbi
Kamanda Chatanda alisema marehemu  aliingia kazini majira ya jioni katika kituo cha polisi wilaya ya kibaha na ni kweli kuwa alikuwa amepangiwa lindo la kwa mkuu wa wilaya ya kibaha.
Alifafanua kwamba  alikutwa na umauti baada ya kujipiga risasi kwa bunduki aina ya smg akiwa anaelekea kwenye lindo  alilopangiwa.
“Alikuwa ndio anaenda lindoni sasa akiwa amekaa mbele ya gari  PT1732 lililokuwa likiendeshwa na F.3064 ,cpl Grayson,ndipo bunduki ilipojifyatua na kumpiga kifuani upande wa kushoto’alisema kamanda Chatanda.
Kamanda Chatanda alisema uchunguzi wa awali umeweza kubaini kuwa marehemu alikuwa ameweka risasi chemba kwenye bunduki aliyokuwa nayo na kwa bahati mbaya akiwa anashuka kwenye gari alilokuwamo ndipo risasi hiyo ilimfyatukia.


 
Copyright © 2014 Mkono Wangu Production Designed by EvMak Tanzania