CURRENT NEWS

Tuesday, November 1, 2016

JAFO AONYA WATAKAOFANYA UDANGANYIFU KWENYE MITIHANI YA KIDATO CHA NNE ILIYOANZA LEO NCHINI.


Naibu Waziri waNchi OfisiyaRais, Tamisemi Selemani Jafo akikagua moja ya chumba kilichoandaliwa kwa ajili ya kufanyiwa Mtihani katika shule ya sekondari ya Kiwanja cha Ndege, mkoani Dodoma.

                    .....................................................................

      Naibu waziri Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi), Selemani Jafo, amefanya ziara kwenye shule mbalimbali mjini Dodoma kuangalia maandalizi kwa ajili ya mtihani wa kidato cha nne unaoanza Leo nchini.

        Katika ziara yake kwenye Shule ya sekondari Jamhuri, Kiwanja cha ndege na Msalato, Jafo amewaonya walimu na wanafunzi hao nchini kuepukana na vitendo vya udanganyifu.

         Akizungumza na walimu na wanafunzi katika shule hizo, Jafo amesema katika mtihani huo hawatarajii kuwepo na udanganyifu kwa kuwa wamejifunza kupitia mtihani wa darasa la saba ambapo kumekuwepo na tabia ya walimu kujificha chooni ili kuwasaidia wanafunzi.


         Amesema shule  zitakazofanya fanya hivyo zitakuwa zimepoteza thamani yake.

        Ameeleza hatarajii mitihani hiyo ifanyike kinyume na kuwataka walimu wasisubutu kufanya udanganyifu wowote na kuziingiza shule zao kwenye kashfa.

                     Jafo amesema mara nyingi mitihani hiyo inapofanyika kumekuwa na wizi wa mitihani na kutofuatwa kwa taratibu za mitihani.

                          Naibu Waziri ofisi ya rais, tamisemi Selemani Jafo akizungumza na wanafunzi watahiniwa katika shule ya sekondari Jamhuri, mkoani Dodoma, alipotembelea kukagua maandalizi ya mtihani wa kidato cha nne unaofanyika leo.Akizungumza na wanafunzi, Jafo amewataka kujiepusha na vitendo hivyo kwa kuwa vitawafali ya awamu ya tano imejipanga kuboresha mazingira mazuri ya kufundishia na kujifunzia na anya wafutiwe mitihani na kupoteza malengo yao kwenye maisha.


Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo akiongozana na  mkuu wa shule ya sekondari ya wasichana Msalato(kulia) Linen Chanafina na watumishi wengine kukagua mazingira katika shule ya hiyo.


 
Copyright © 2014 Mkono Wangu Production Designed by EvMak Tanzania