Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tamisemi, Selemani Jafo akisaini kitabu cha wageni shule
ya sekondari Segera, kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya
Handeni Wiliam Makufwe na kulia ni Mkuu
wa Wilaya ya Handeni Godwin Gondwe.
Picha ya
pamoja ya Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo na walimu wa shule ya sekondari
ya Segera.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni William Makufwe akitoa utambulisho
mfupi kwenye ukumbi wa Halmashauri.
.............................................................................
Naibu Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi),Selemani
Jafo amewataka maafisa elimu kupanga muda wa kusikiliza kero za walimu na
kuzitafutia ufumbuzi ili kuongeza morali ya walimu kufundisha.
Jafo ametoa
agizo hilo alipokuwa akiongea na walimu wa shule ya sekondari Segera iliyopo
wilayani Handeni, katika ziara yake aliyoifanya Wilayani Handeni na Mkoa wa
Tanga.
Amesema wapo baadhi ya Maafisa elimu ambao wanajifanya kuwa ni Miungu watu linapokuja suala la kusikiliza na kutatua kero za walimu.
“Najua wapo wapo
walimu wanaotembea umbali mrefu kufuata huduma makao makuu ya Halmashauri kwa
wakubwa wao mara nyingi wameshindwa kutatuliwa kero zao hali inayopelekea
usumbufu, Kuanzia leo napiga marufuku tabia hiyo,”amesema Jafo.
Amesisitiza Maafisa
elimu hao wapo kwa lengo la kuwasikiliza walimu na kuwasaidia kutatua kero zao
ili waweze kujikita katika ufundishaji wa wanafunzi.
Kadhalika,
amebainisha walimu ni watu muhimu sana nchini ila wamekuwa wakikatishwa tamaa
na utendaji wa baadhi ya maafisa elimu.
Ameongeza
kuwa kero kubwa ya walimu ni kutokupanda madaraja kwa wakati na kutopata
stahiki zao ikiwa ni pamoja na posho za likizo,uhamisho na madai mengine.
Katika hatua nyingine, Naibu Waziri Jafo ameagiza Halmashauri ya Wilaya ya Handeni kukamilisha miradi yote ya SEDP-II ambayo haijakamilika kuhakikisha inakamilika kabla au ifikapo desemba 20, mwaka huu.
Katika hatua nyingine, Naibu Waziri Jafo ameagiza Halmashauri ya Wilaya ya Handeni kukamilisha miradi yote ya SEDP-II ambayo haijakamilika kuhakikisha inakamilika kabla au ifikapo desemba 20, mwaka huu.
“Katika
kusimamia miradi hiyo na miradi ya maendeleo kwa ujumla kila mtu lazima atimize
wajibu wake na kuhakikisha fedha iliyotengwa na kutolewa inatumika vizuri na
thamani fedha (value for money) inaonekana,”amesema Naibu Waziri Jafo.
Baadhi ya
watumishi wa halmashauri ya Handeni.
Viongozi wakisikiliza kwa makini maagizo ya
Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Selemani Jafo.
Post a Comment