CURRENT NEWS

Friday, November 11, 2016

MADAKTARI BINGWA 17 WA SAUD ARABIA KUTUA ZANZIBAR NOV 11

Balozi Hemed Mgaza kushoto alipokwenda kujitambulisha kwa Rais wa Zanzibar, Dkt Mohamed Ali Shein akiwa nchini Tanzania. Picha na Maktaba.
Na Mwandishi Wetu, Saudi Arabia
JOPO la Madaktari Bingwa 17 kutoka nchini Saudi Arabia, wanatarajiwa kuwasili Zanzibar Novemba 11 kwa ajili ya kuweka kambi ya kutoa matibabu (Medical Camp) katika Hospitali za Chake Chake na Wete kwenye Kisiwa cha Pemba.
Programu hii inaratibiwa na Jumuiya ya Kimataifa ya Vijana wa Kiislamu ya Saudi Arabia World Assembly of Muslim Youth – WAMY kwa ajili ya kwenda nchini Tanzania katika kisiwa cha Pemba kutoka huduma hiyo ya afya.
Akizungumza mjini hapa, Balozi wa Tanzania nchini Saud Arabia, Hemed Mgaza, alisema kwamba msafara wa madaktari hao utakuwa na tija kwa Watanzania wote, hususan wa Kiwa cha Pemba.
Alisema kwamba taratibu zote za madaktari hao zimekamilika, huku ratiba yao ikionekana kwamba watahudumia kuanzia Novemba 11 hadi 22 kabla ya kuekea na ratiba zao ambapo ni jambo la kujivunia kwa wataalam hao kuamua kwenda nyumbani Tanzania kutumia taaluma zao.
“Madaktari hao watatoa huduma ya matibabu kwa muda wa siku kumi bila malipo kuanzia tarehe 11 hadi 22 mwezi Novemba, 2016 kama taarifa za msafara wao zinavyoonekana katika ofisi zetu.
“Pamoja na kutoa huduma za matibabu, Madaktari hao watakwenda na dawa na vifaa tiba vya aina mbalimbali ambavyo mwisho wa kambi hiyo watavitoa msaada kwenye hospitali hizo,” alisema.
Kwa mujibu wa Balozi Mgaza, ujio wa madaktari hao ni wa mara ya kwanza nchini Tanzania na wanatarajia kutoa huduma hizo sehemu nyingine za Tanzania siku zijazo baada ya kukamilisha awamu ya kwanza, huku madaktari hao wakiwa wameshatoa huduma kama hizo katika nchi za Comoro, Cameroon na kwingineko
 
Copyright © 2014 Mkono Wangu Production Designed by EvMak Tanzania