CURRENT NEWS

Monday, November 14, 2016

MAKAMU WA RAIS ASAFIRI NA BOMBARDIER Q400 NEXTGEN KUTOKA DAR MPAKA MWANZA

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipokea tiketi ya kusafiria muda mfupi kabla ya kusafiri kuelekea Mwanza na abiria wa kawaida kwa ndege mpya ya Bombardier Q400 NextGen kutoka kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbalawa(kushoto) na Mkurugenzi wa Shirika la Ndege Tanzania Mhandisi Ladisaus Matindi.


  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na waandishi  wa habari muda mfupi kabla ya kupanda ndege mpya za Bombardier Q400 NextGen kuelekea mkoani Mwanza kwenye ziara ya kikazi.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na wafanya kazi wa ndege mpya za Bombardier Q400 NextGen kuelekea mkoani Mwanza kwenye ziara ya kikazi.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwasalimu abiria waliosafiri nae kwenye ndege mpya ya Bombadier Q400 ya shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) akitokea Dar es Salaam kuelekea jijini Mwanza kwa ziara ya kikazi.
                                           ........................................................


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amewasili jijini Mwanza na kwa mara ya kwanza umetumia usafiri ya ndege ya Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) aina ya bombardier Q400 kutoka Dar es Salaam hadi Mwanza ambapo ndege hiyo pia ilibeba abiria wa kawaida katika safari hiyo.


Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan akizungumza na waandishi wa habari katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam kabla ya kusafiri na baada ya kuwasili mkoani Mwanza amewahimiza wananchi kutumia usafiri wa ndege za ATCL kwa sababu ni wa bei nafuu na usafiri wake ni wa uhakika.

Amesema kwa kutumia ndege ya ACTL imemsaidia kupunguza gharama kubwa ya usafiri kwa kutumia ndege za binafsi za kukodi kwa ajili ya safari za kikazi za ndani ya nchi.


“Ni ndege zetu ni fahari yetu zipo Tanzania ni lazima sisi Watanzania tuzitumie ipasavyo kusafiria ndio maana na mimi leo nimeamua kutumia usafiri wa ATCL kwa sababu ni mzuri na wa uhakika


Makamu wa Rais amesema amefurahi kusafiri kwa mara ya kwanza na ndege hiyo kutoka Dar es Salaam hadi Mwanza na amehimiza viongozi na wananchi kwa ujumla kutumia usafiri wa ndege za ATCL ili kulipa nguvu shirika hilo katika ufanyaji wake wa kazi kwa viwango bora zaidi.


Mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege mkoani Mwanza, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amepokelewa na viongozi mbalimbali wa serikali na wa vyama vya siasa ambao waliongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongella.


Akiwa mkoani Mwanza, Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan atafanya ziara ya kikazi siku NNE mkoani humo katika  wilaya za Ukerewe,Ilemela,Nyamagana, Misungwi,Kwimba na Magu.


 
Copyright © 2014 Mkono Wangu Production Designed by EvMak Tanzania