CURRENT NEWS

Thursday, November 10, 2016

MOTO MKUBWA WATEKETEZA BOHARI LA KAMPUNI YA 7 GENERAL ENTERPRISES MIKOCHENI JIJINI DAR ES SALAAM
Hivi ndivyo moto mkubwa ulivyokuwa ukiwaka katika Bohari la 7 General Enterprises ambapo walikuwa wakihifadhia Mataili, mchana eneo la Mikocheni Jijini Dar es salaam.

Vikosi mbalimbali vya zima moto kutoka Serikali na Makampuni binafsi wakiendelea na juhudi za kuuzima moto huo.

Baadhi ya watu mbalimbali wakiendelea kushuhudia tukio hilo la kuteketea kwa Bohari

Moto Mkubwa ukiendelea kuwaka


Kamanda wa Polisi Mkoa wa kipolisi wa Kinondoni Suzan Kaganda akizungumzia kwa ufupi tukio hili na kusema kuwa kwa sasa hawezi zungumza chochote mpaka moto utakapozimwa kabisa


Hapa mpaka Trekta nalo lilihusika katika kuhakikisha moto huo unazimika

Mmoja wa waandishi wa Habari ambaye hakujulikana anatokea katika chombo gani akiwa anaendelea kutafuta sehemu nzuri ya kuchukua taarifa.

Baadhi ya wataalam wa kuzima moto wakiwa wanaendelea na juhudi za kutazama maeneo ambayo moto unawaka zaidi ili kuuzima

Moja ya Gari la zima moto likiwa linawahi eneo la Tukio kusaidia kuzima moto
Zima moto wakiendelea na shughuli ya kuhakikisha moto unazimika katika Bohali hilo

Moto ukiendelea kuteketeza Bohari hilo lililokuwa la kuhifadhia mataili

Pamoja na watu kupewa tahadhali ya Moto mkubwa uliokuwa unawaka lakini bado walikuwa wakiongezeka kushuhudia tukio hilo.

Katika juhudi za kuhakikisha moto huo unazimika kabisa magari ya kila aina yanayobeba maji yalichukuliwa kuongeza nguvu za kuzima moto huo.

Ulinzi ukiwa umeimarishwa kabisa katika eneo ambalo moto ulikuwa unawaka

Mmoja wa wafanyakazi wa Bohari hilo Shaban Salum akielezea kwa ufupi kile alichokiona wakati moto huo unaanza kuwaka mida ya saa sita mchanaMagari ya zimamoto na mengine ambayo ni ya kubebea maji yakiwa katika eneo la Bohali la 7 General kuhakikisha wanashirikiana kumaliza moto huo


Umati wa watu wakiwa katika eneo hilo la Bohari wakiendelea kushuhudia Tukio hilo

Watu wengine wakiwa wamekaa Jirani kabisa na Moto huo bila wasiwasi wakishuhudia tukio hilo la Moto.


Taarifa kamili itakuja kutoka Jeshi la Polisi


Picha zote na Fredy Njeje/Blogs za mikoa
 
Copyright © 2014 Mkono Wangu Production Designed by EvMak Tanzania