CURRENT NEWS

Saturday, November 5, 2016

MUSWADA WA SHERIA YA HUDUMA ZA HABARI WASOMWA MARA YA PILI
Na Eleuteri Mangi- MAELEZO

Muwada wa Sheria ya Huduma za Habari wa mwaka 2016 umesomwa mara ya pili Bungeni mjini Dodoma ukiwa na lengo la kuifanya tasnia ya habari nchini kuwa taaluma kamili.

Wiziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Nape Nnauye amesema hay oleo Bungeni Dodoma alipokuwa akiwasilisha Muswada huo, huku akisisitiza kuwa una sehemu kuu nane ambazo zinaufanya kuleta mageuzi katika tasnia ya habari nchini na kuifanya kuwa taaluma kamili itayowaletea heshima wanahabari na tasnia hiyo kwa ujumla. 

“Hatuwezi kwa na vyombo vya habari makini kama hatutakuwa na wanahabari wenye taaluma ya habari nchini” alisema Nape.

Katika kuonesha ushirikishwaji wa wadau katika kutoa maoni yaliyolenga kuboresha Muswada huo, Waziri Nape amesema kuwa kumekuwa na ushirikishwaji mkubwa wenye wigo mpana kutoka kwa mwananchi mmoja mmoja, wanataaluma wa habari, wanasheria kupitia Chama cha Mawakili Tanzania (TLS), Baraza la Habari Tanzania (MCT), Umoja wa Wamiliki wa vyombo vya habari (MOAT) na Taasisi ya Wanahabari Kusini mwa Afrika, tawi la Tanzania (MISA-TAN).

Wadau wengine walitoa maoni yao ni Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Sikika, Wabunge kupitia Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii pamoja na michango ya Wabunge kupitia Kamati nyingine ambao umesaidia katika kuboresha Muswada huo wenye dhamira ya kuleta ufanisi katika sekta ya habari. 

Miongoni mwa maeneo ambayo wadau hao wameyafanyia maboresho ili Muswada uwe na tija ni pamoja na kuainisha haki na wajibu wa wananhabari ikiwemo uhuru wa kukusanya, kuhariri na kuchapisha au kutangaza habari pamoja na kuainisha haki ya chombo cha habari kukata rufaa kwa kuzingatia mfumo wa wazi na wa kidemokrasia kupitia vyombo vya kutoa haki ikiwemo mahakama huku Jaji Mkuu akiweka utaratibu wa kusikilizwa haraka kwa kesi za masuala ya kihabari.

Maboresho mengine yaliyofanya ni uwakilishi wa wanahabari katika Bodi ya Ithibati kwa kuzingatia uwiano wa wajumbe kutoka sekta ya habari ya umma na ya binafsi, kuviondolea adhabu vyombo vya habari au wamiliki baadhi ya makosa ya mwandishi ambapo atawajibishwa na Bodi ya Ithibati akiwa yeye ni mwanataaluma kamili kukutenda makosa ya kimaadili na vyombo vya dola kukamata mitambo na vifaa vya wanahabari maboresho yanaonesha kazi hiyo sasa itafanywa na Jeshi la Polisi kwa sheria ya Mwenendo wa Mkosa ya Jinai badala ya kazi hiyo kufanywa na Mkurugenzi wa Idara ya Habari. 

Zaidi ya maboresho hayo, Waziri Nape ameongeza kuwa maboresho mengine ni kuhusu mitambo kutohusika moja kwa moja kwa kosa la gazeti ambalo limechapisha habari yenye makosa ya kisheria dhidi ya watu au taasisi mbalimbali.

Waziri Nape amefafanua kuwa chimbuko, muktadha na mchakato wa kuandaa Muswada huo unatokana na baadhi ya vipengele vya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania baada ya kufanyiwa marekebisho mwaka 1984 ambapo haki ya kikatiba ya kutafuta, kupokea na kutoa habari imeainishwa kwenye Ibara ya 18 (b) pamoja na mikataba mbalimbali ya kimataifa ya inayoainisha haki na wajibu wa sekta ya habari. 

Mkatabahiyo ya Kimataifa ni ule wa Haki za Kisiasa na Kiraia wa mwaka 1966 ambao Tanzania iliuridhia Juni 11, 1984 pamoja na Mkataba wa Afrika wa Haki za Binadamu na Watu 1981 ambao nao uliridhiwa Februari 18, 1984.

Akinukuu maneno mbalimbali ya watu maarufu duniani juu ya masuala ya habari akiwemo Rais wa Marekani Thomas Jefferson Januari 16, 1789, Rais wa zamani wa Afrika Kusini Nelson Mandela, Muasisi wa Taifa la India Mahatma Ghandhi, Baba wa Uhuru wa Habari John Stuart Mill (1806-1873) pamoja na Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere, Waziri Nape akinukuu maneno ya mmoja wa viongozi hao Mahatma Ghandhi aliamini kuwa uhuru wa kweli wa kujieleza ni ule unaoweka mbele heshima ya watu wengine na kuwalinda dhidi ya dhara, kebehi, kejeli na madhara mengine huku Baba wa Uhuru wa Habari John Stuart Mill akibainisha dhima ya uhuru wa vyombo vya habari na umuhimu wa kuwa huriu unapaswa kuzingatia ukomo wa haki ya kupata habari kuwa unakoma pale haki za watu wengine zinapoanzia.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii Peter Serukamba amesema kuwa kamati yake imeufanyia kazi Muswada huo kupitia maoni ya wadau na watu mbalimbali nchini ambayo ndio yamakuwa msingi wa kuuboresha muswada huo.

Serukamba aliongeza kuwa kati ya miswada ambayo wananchi wengi wameisoma na kusikilizwa ni Muswada habari ambao umejadiliwa kwa njia mbalimbali ikiwemo vyombo vya habari; kwenye magazeti, kwenye radio na Televisheni kupitia vipindi maalum vya kujadili Muswada huu na maoni yao mengi yameingizwa kwenye Muswada huu” alisema Serukamba.
 
Copyright © 2014 Mkono Wangu Production Designed by EvMak Tanzania