CURRENT NEWS

Wednesday, November 23, 2016

MWIGULU AWAONYA MADEREVA WANAOACHA MAGOGO,MAWE BARABARANI


Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mwigulu Nchemba akiwa na viongozi wengine wa mkoa wa Singida katika kikao cha Bodi ya barabara ya mkoa huo.

                                     ...............................................................
WAZIRI  wa Mambo ya ndani ya Nchi Mwigulu Nchemba amekemea madereva wanaoacha mawe na magogo barabarani baada ya kutengeneza magari yao huku wakamatwe kila wanapobainika kufanya kosa hilo.

Mwigulu ametoa kauli hiyo Novemba 22, mwaka huu  katika kikao cha Bodi ya barabara mkoa wa Singida.

Akizungumza katika kikao hicho, amesema tabia hii imeshamiri kwa baadhi ya madereva kuweka mawe makubwa, magogo au matawi ya miti punde magari yanapokuwa yameharibika.

“ Kibaya ni kwamba wanapotengeneza magari yao huyaacha mawe au magogo katikati ya barabara na kuondoka zao. Hali hii imekuwa ikisababisha ajali na imekuwa chanzo kikuu cha uharibifu wa barabara.

Ameongeza "tuwe wastaarabu na wazalendo katika matumizi ya barabara, kuna madereva wanaweka Mawe na Magogo makubwa barabarani wanapoharibikiwa na magari, wakishatengeneza wanaondoka bila kuondoa mawe hayo au magogo hayo, huu sio uungwana, tabia hii inaharibu barabara zetu zilizojengwa kwa gharama kubwa na ni chanzo cha ajali"

Amesema hatua hiyo ni si ustaraabu huku akifafananisha na mtu aliyejisaidia na kuacha choo bila kuflash.

Ameagiza Askari kuchukua kumbukumbu kila magari yanapoharibika na watakapoondoka bila kuondoa mawe wawasiliane popote watakapokuwa wamefika wakamatwe na wafike kwenye mkono wa sheria kwa hali hiyo inasababisha kutengeneza mazingira ya ajali na kuharibu barabara. 
Copyright © 2014 Mkono Wangu Production Designed by EvMak Tanzania