CURRENT NEWS

Saturday, November 26, 2016

JAFO AWAKOMALIA WAHANDISI WA HALMASHAURI ZA MKOA WA TANGA KWA KUTOZINGATIA MAHITAJI YA WANAFUNZI WALEMAVU

                   
Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi), Selemani Jafo akizungumza na watumishi wa wilaya ya Handeni ikiwa ni sehemu ya ziara yake aliyoifanya Mkoani Tanga.
watumishi wakimsikiliza Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi), Selemani Jafo.

...........................................................................................

Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi), Selemani Jafo amehitimisha ziara yake Mkoani Tanga huku akionesha kuchukizwa na kitendo cha Wahandisi wa ujenzi Katika Halmashauri za mkoa huo kwa kutozingatia mahitaji ya wanafunzi wenye ulemavu.

Jafo alifanikisha ziara yake ya siku tatu kwa kutembelea Halmashauri zote za mkoa wa Tanga.

Katika ziara yake mkoani huo, Jafo alikagua ujenzi wa vyoo vinavyo jengwa katika shule mbalimbali za sekondari mkoani Tanga kupitia mradi wa SEDEP II.

Akizungumza mara baada ya ziara yake, Jafo alisema amegundua vyoo vyote vilivyo kamilika na vinavyo endelea kukamikishwa mkoani huo havijazingatia kuweka miundombinu ya watu wenye ulemavu.

“Katika kila shule niliyopita nimekuta vyoo vizuri sana vimejengwa lakini vina kasoro ya kukosa hata tundu moja kwa maeneo yote ya wasichana na wavulana yaliyo andaliwa kwaajili ya watoto walemavu,”alisema Jafo

Aliwaagiza wakurugenzi wote kuhakikisha hitaji hilo la msingi kwa watoto walemavu linazingatiwa kwa kufanya marekebisho kwa upande wa vyoo vya wavulana na wasichana ili kupata tundu moja kwa lengo la kuwasaidia watoto wenye ulemavu.

Jafo mara baada ya kuhitimisha ziara yake mkoani Tanga anaelekea kuanza ziara nyingine katika mkoa wa Ruvuma, Mtwara, Lindi na Pwani.
 
Copyright © 2014 Mkono Wangu Production Designed by EvMak Tanzania