CURRENT NEWS

Thursday, November 3, 2016

PSPF YAONGEZA WANACHAMA WAPYA 50,185 KWA KIPINDI CHA MWAKA MMOJA.


Na Tiganya Vincent-MAELEZO

Novemba 5, mwaka huu ni mwaka mmoja tangu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli alioapishwa kuwa kiongozi  na Amri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama wa nchi hii.

Katika kipindi cha mwaka mmoja cha utawala wa Rais Magufuli nchini, Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSPF) kwa upande wake umesaidia Watanzania wanaopata huduma za Jamii kupitia PSPF kuongezeka kutoka 394,494 hadi kufikia 444,679 ikiwa ni sehemu ya utekeleza wa agizo lake.

Hatua hii ya PSPF imelenga kutekeza agizo na kutimiza ahadi ya Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania aliyokuwa akitoa ya kuhakikisha kuwa Watanzania wengi wanufaika na huduma za Hifadhi za Jamii ikiwemo huduma za Bima za afya wakati wa kampeni na baada ya kuingia madarakani.

Kwa mujibu wa taarifa ya mwaka mmoja kwa upande wa Mfuko wa PSPF iliyotolewa na Costantina Martin kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa PSPF ,idadi hiyo hii inajumuisha Watanzania walio katika sekta rasmi na isiyo rasmi nchini.

Kundi hili kubwa lilikuwa limesaulika kujumuishwa katika hifadhi ya jamii , lakini baada ya Mhe. Rais Magufuli kulizungumzia katika kampeni zake hivi sasa mwamko wa kujiunga na hifadhi ya jamii umeongezeka na PSPF imeanza kulitekeleza agizo hilo kwa kuwahamasisha wananchi waliopo katika sekta isiyo rasmi na sekta rasmi kuchangia na kujiunga katika Bima ya Afya.

Katika kuhakikisha kuwa azma hiyo inatimizwa tayari PSPF imeingia makubaliano na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya(NHIF) kwa lengo la kufikisha huduma za afya kwa watanzania wengi ambao wapo katika sekta isyo rasmi na hivyo kujenga jamii yenye afya bora inayochangia katika ujenzi wa nchi.

Chini ya makubaliano yanawasaidia wanachama wa PSPF walio katika Mpango wa Uchangiaji wa Hiari kuweza kupata ya tiba kupitia NHIF kwa gharama ya shilingi 76,800/- kwa mwaka katika hospitali mbalimbali ziliingia makubaliano na Mfuko huo wa Bima ya Afya.
Mpango huo wa PSPF unaounga mkono juhudi za Rais Magufuli  za kutaka kuhakikisha kuwa wananchi wengi wanapata huduma na matibabu nchi nzima kwenye vituo vyote vilivyosajiliwa na NHIF kuanzia Zahanati hadi Hospitali ya Taifa kwa gharama nafuu.

Hivi sasa huduma hiyo ya PSPF kuwadhamini wananchama wake kwa ajili ya kupata matibabu imesaidia watanzania wengi sana kunufaika na huduma hii husasan katika kipindi cha mwaka mmoja wa Rais Magufuli.

Akifungua rasmi Bunge la 11 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania , Rais Magufuli alisema kuwa dhamira ya kujenga uchumi wa kisasa na suala la kupambana na umaskini linakwenda sambamba na kuwa na wananchi wenye afya bora.

Aliongeza kuwa Serikali ya Awamu ya Tano itahakikisha wananchi wanapata huduma bora za afya kwa kuhamasisha wananchi wengi wanajiunga na Bima ya Afya.

Katika kutekeleza hilo PSPF kwa kushirikiana na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya(NHIF) imeshawafikia Watanzania 2,710 walio katika sekta isiyo rasmi kuanza  kunufaika na huduma za Afya kupitia PSPF.

Mbali na sekta ya afya , katika kipindi cha mwaka mmoja wa Rais Magufuli PSPF kwa upande wake imesaidia kuhakikisha kuwa Tanznaia inakuwa Nchi ya Viwanda kwa lengo la kutoa ajira kwa Watanzania walio wengi.

Viwanda hivyo ambavyo PSPF imewekeza ni pamoja na 21st Century cha Morogoro, Saruji Tanga.
Martin ameongeza kuwa hivi sasa PSPF imejipanga kuwekeza katika Kituo cha Biashara cha Kurasini (Kurasini Logistic Center) kwa lengo la kuchochea uwekezaji wa viwanda na kutoa ajira kwa wananchi.

Viwanda vingine ambavyo PSPF imejipanga kuwekeza ni kile cha Nguo cha Urafiki, Morogoro Canvas Mill na Kiwanda cha Viatu Karanga kilichopo Moshi.

Hatua hiyo iliyoanza kutekelezwa na PSPF ni sehemu utekelezaji hotuba ya Mhe. Rais Magufuli wakati anafungua rasmi Bunge 11 mjini Dodoma mwishoni mwa mwaka jana ambapo alisema kuwa Serikali ya Awamu ya Tano itaweka mkazo katika ujenzi wa viwanda ili mwaka 2020 idadi ya ajira itokanayo na viwanda ifikie asilimia 40 ya ajira zote hapa nchini.

PSPF ilianzishwa kwa sheria ya Mafao ya Hitimisho la Kazi kwa Watumishi wa Umma namba 2 ya mwaka 199 . sura ya 371 na inatoa huduma za Hifadhi ya Jamii katika Mapngo wa lazimana wa hiyari.

Mwisho
 
Copyright © 2014 Mkono Wangu Production Designed by EvMak Tanzania