CURRENT NEWS

Wednesday, November 30, 2016

PWANI YASHUKA MATOKEO YA DARASA LA SABA KITAIFA

Kaimu katibu tawala mkoani Pwani,Edward Mwakipesile,akizungumza akionekana akizungumzia jambo,katika mkutano wa kuchambua na kutangaza matokeo ya mtihani wa wanafunzi waliomaliza darasa la saba kimkoa ,mwaka huu.(Picha na Mwamvua Mwinyi)
MKOA wa Pwani umeshuka katika ufaulu wa matokeo ya mtihani wa kumaliza darasa la saba mwaka huu kutoka asilimia 63.1 mwaka 2015 na kufikia asilimia 62.5 mwaka 2016 na kusababisha kushika nafasi ya 21 kitaifa .
Aidha wanafunzi 15,528 mkoani hapo wamefaulu kwenda kujiunga na shule za sekondari  mwaka 2017 baada ya kufanya mtihani huo.
Hayo yalisemwa na kaimu afisa elimu mkoa wa Pwani ,Modest Tarimo wakati wa uchambuzi wa matokeo ya mtihani wa kuhitimu elimu ya msingi mwaka 2016 mkoa . 
Tarimo alisema matokeo hayo hayaridhishi kutokana na ufaulu kushuka badala ya kupanda licha ya kushuka kwa asilimia 0.5 ukilinganisha na matokeo ya mwaka jana.

Hata hivyo alieleza kwamba kati ya wanafunzi aliofanya mtihani 24,818, wanafunzi 9,290 wamefeli sawa na asilimia 37.4 .
“Wanafunzi wote waliofaulu wamechaguliwa kujiunga na elimu ya sekondari ambapo wamefaulu kwa kupata alama zaidi ya 100 kati yao 288 wamepata daraja la A.
“Wanafunzi 2,636 walipata daraja B, wanafunzi 12,604 wamepata daraja C na wote waliopata daraja A na C wote wamechaguliwa kujiunga na sekondari”alisema Tarimo.
Katika hatua nyingine Tarimo alifafanua kuwa, wanafunzi waliokuwa wakitarajiwa kufanya mtihani walikuwa 24,913 lakini waliofanya ni 24,818 wavulana wakiwa ni 11,334 na wasichana walikuwa ni 13,484 sawa na asilimia 99.9.
Tarimo alisema watahiniwa 95 hawakufanya mtihani sawa na asilimia 0.3 kutokana na sababu mbalimbali ikiwa ni pamoja na utoro, wanafunzi 75, mimba mwanafunzi mmoja, vifo 11, ugonjwa wawili na sababu nyingine sita.
Kaimu katibu tawala wa mkoa wa Pwani, Edward Mwakipesile aliserikali iliweka wastani wa asilimia 80 ya ufaulu kwa shule za msingi ikiwa ni mkakati wa kufikia mpango wa matokeo makubwa sasa (BRN).

Alisema kufuatia mkakati huo kuna kila sababu ya wadau wa elimu kupiga vita utoro ambao umepungua  sambamba na kusimamia watoto wa kike ili kujiepusha na mimba za utotoni.

Mwakipesile aliwataka wadau hao na jamii kushirikiana na idara ya elimu wilaya na mkoa kukabiliana na changamoto zinazosababisha ufaulu kushuka ili kuhakikisha matokea ya mwaka ujao .
 
Copyright © 2014 Mkono Wangu Production Designed by EvMak Tanzania