CURRENT NEWS

Sunday, November 27, 2016

SERIKALI MUFINDI YASIFU SHULE YA ENGLISH MEDIUM YA SOUTHERN HIHGLAND MAFINGA ,YATAKA WALIMU WOTE KUIGA MFANO KWA SHULE HIYO ......Mjumbe  wa bodi  ya  shule ya  English Medium ya  Southern Highlands Mafinga  Marcelina Mkini ambae ni mjumbe wa NEC Taifa  akipata  maelekezo kutoka kwa  wanafunzi wa  shule  hiyo alipotembelea darasa la mafunzo ya  kompyuta

Baadhi ya  walimu wakijitambulisha kwa  waalikwa
Baadhi ya  wazazi  wakipata  maelezo kwa wanafunzi hao
Wazazi  wakitazama  jinsi wanafunzi hao  walivyobobea katika kompyuta
Wanafunzi wa Chekechea 31  waliohitimu wakionyesha maonyesho ya masomo
Wanafunzi  wa shule  hiyo  wakionyesha maonyesho ya masomo wakati wa mahafali ya  chekechea
Baadhi ya  wazazi  waaosomesha  watoto  wao shule ya  Southern Highlands Mafinga
Mkuu wa  shule ya  Southrn Highlands Mafinga  Joson Nyangwara akisoma  taarifa ya  shule  hiyo mbele ya  wazazi 
Wanafunzi  wa  chekechea  wakisoma  risala yao
Mjumbe  wa  bodi ya  shule ya  English Medium ya  Southern Highlands Mafinga mkoani Iringa Marcelina Mkini  akimpongeza mmoja kati ya  wanafunzi wa  shule   hiyo kwa kufanya  vizuri katika masomo yake jana  wakati wa mahafali ya Chekechea na  kikao  cha wazazi shuleni hapo
Diwani  wa Luhunga  kushoto  akiwa na diwani wa kasanga  baada ya  kukutana  shule ya  Southern Highlands Mafinga  kushiriki kikao  cha wazazi
Magari ya  baadhi ya  wazazi wanaosomesha  watoto wao  shule ya Southren Highlands Mafinga yakiwa  yameegeshwa nje ya shule  hiyo
style="clear: both; text-align: center;">

Mgeni  rasmi  Daniel Mwaisela akikabidhiwa  zawadi  toka kwa  uongozi wa  shule ya  Southern Hihglands Mafinga 
Na MatukiodaimaBlog 
SERIKALI  wilayani Mufindi  mkoani  Iringa   imepongeza kasi  ya ufundishaji ya walimu wa shule binafsi ya Southern Highlands Mafinga na kuwataka  walimu  wa  shule zote kuiga mfano  wa walimu wa shule ya  southern Highlands Mafinga ili  kuiwezesha wilaya  hiyo  kuwa  na shule bora nyingi  zaidi .Kuwa  jitihada zinazoonyeshwa na walimu wa shule ya Southern Highklands Mafinga ambazo zimekuwa  zikiifanya  shule hiyo kuendelea kuongoza mitihani ya Kitaifa ya darasa la saba kila mwaka zinapaswa kuonyeshwa na walimu wa shule nyingine wilayani hapo  ili kuipa heshima wilaya na mkoa wa Iringa  .Akitoa pongezi  hizo jana  kwa niaba ya mkuu wa wilaya mgeni rasmi katika  sherehe za mahafali ya chekechea na kikao cha  wazazi katika shule   hiyo ya  Southern Highlands Mafinga   katibu tarafa wa Ifwagi   Arois Mtengella  alisema wilaya inajivunia sana na matokeo mazuri ya shule  hiyo.

                                                                                             

“Shule  hii ambayo ni English  Medium   imekuwa  ikifanya vizuri   sana katika  mitihani yake na  kitendo  cha   wazazi kutoka nje ya wilaya na mkoa  wa Iringa  kuleta  watoto  wao hapa Mafinga  ni moja ya mambo ya  kujivunia  …..pia uchumi  wa wilaya  yetu  unaongezeka kwa  wageni hao kuja hapa kwetu maana siku kama  hii kila mwananchi mwenye biashara ameingiza  kipato chake”Pia  alisema  changamoto kubwa kwa  wilaya  ya  Mufindi na mkoa  wa Iringa  pamoja na  kuongoza kwa uzalishaji wa mazao ya chakula kama mahindi  ila  bado  watoto  wengi  wanatatizo  la utapiamlo hivyo   kuwataka  wananchi  kuongeza  jitihada za  kuwapikia  watoto  wao ugali  wa  dona badala ya  kukomboa mahindi .Alisema   kitendo cha  watoto  kulishwa ugali  wa mahindi  yaliyokobolewa na  kulowekwa  ni  kuwafanya  kuwa na afya duni na  hivyo  uwezo  wao darasani  huwa mdogo  zaidi .Mkuu  huyo  wa wilaya  alisema  kuwa  elimu  bora ni  pamoja na  lishe  nzuri kwa  watoto na  kuwa  wazazi  lazima  wahakikishe   watoto  wao  wanawapa lishe bora ili  kuwaongezea   uwezo  wa  kufundishika .

                              

Kwa upande  wake mwalimu mkuu wa Southern Highlands Mafinga Joson Nyangwara  akizungumza kwa niaba ya mkurugenzi mtendaji wa shule hiyo Mary Mungai alisema kuwa  shule   imekuwa na utaratibu  wa  kukutana na wazazi na  walezi wa  wanafunzi  wanaosoma shuleni hapo  mara  baada ya  matokeo ya kitaifa ya mtihani wa  darasa la  saba   ili kupokea  maoni yao mbali mbali  kwa ajili ya  maendeleo ya shule  hiyo .Mkuu  huyo  alisema  moja kati ya mafanikio ya  shule  hiyo  kuendelea  kufanya  vizuri  katika mitihani ya  taifa ya  darasa la  saba  kila mwaka ni kutokana na ushirikiano  mzuri  uliokuwepo kati ya  wazazi na  walimu na  kuwa  kupitia  vikao vya pamoja kati ya  wazazi na uongozi  wa  shule mapungufu  yanayojitokeza yamekuwa  yakifanyiwa  kazi pasipo  watoto  kupata  vikwazo  katika masomo  yao.Hivyo  alisema kwa mwaka huu   wanafunzi wote   51 waliofanya mtihani wa Taifa wa darasa la  saba wamefaulu kujiunga na kidato cha kwanza mapema mwakani  jambo  ambalo linaendelea kuwavuta wazazi  wengi  zaidi kupeleka  watoto wao shuleni hapo .


 Kuwa  mwaka huu 2016 jumla ya wanafunzi 51 walisajiliwa  kufanya mtihani wa  darasa la  saba na  wote  walifanya wastani wa  shule 185.3137 kundi  la shule  watahiniwa 40 au  zaidi ambapo imeweza  kuongoza kiwilaya kuwa ya kwanza na kimkoa ya 6 kati ya shule 232 katika  mkoa  wa Iringa na shule ya 198 kati  ya shule 8109 kitaifa .Alisema  kuwa  toka  shule  hiyo  ilipoanzishwa mwaka 1994 kama Day Care na Pre-school na mwaka 1997 kuanza shule ya msingi imekuwa ikifanya  vizuri na hakuna mtoto aliyepata  kufeli .“Shule  yetu mwaka 2001 shule ilitoa wanafunzi wa kwanza wa darasa la Saba na wanafunzi walikuwa 17, wote walifaulu vizuri na wote walichaguliwa kuendelea na masomo ya kidato cha kwanza” Shule    hiyo inapenda  kuwatangazia   wazazi  kote  nchini ambao  wanatafuta shule  bora kwa  ajili ya watoto  wao kuwa  nafasi  bado  zipo na  kuwa  wanapokea  watoto  wa chekechea ,darasa kwanza ,pili ,tatu na tano  wanaotoka  shule za kawaida kiswahili au English medium


kwa  darasa  la nne na  sita lazima  wawe  wanatoka shule  za  english medium tu 

usahili  unafanyika  tarehe 10/12/2016 shuleni Mafinga  na  baada ya hapo  itakuwa  kila  siku ya kazi kuanzia saa 2 asubuhi  hadi saa 9 alasiri 

fomu  zinapatikana shuleni Southern Highlands Mafinga mjini au katika tovuti ya  shule www.southern Highlands.ac.tz kwa maelezo  zaidi  piga  simu  0754651966 ,0752 840884 au 0756749151
Mjumbe  wa  bodi  ya  shule  hiyo Marcelina Mkini alisema kuwa  kwa  ajili ya uwekezaji  wa kweli ni  vizuri  wazazi  kuwekeza  pesa  zao kwa  kusomesha  watoto badala ya  kuweka pesa  benk

Alisema  kuweka  pesa  benk pasipo  kusomesha  watoto ni  bure kwani mwisho  wa  siku fedha   hizo  huleta ugomvi wakati  mzazi unapokufa ndugu  huanza  kugombaniana na  kuwaacha  watoto masikini.


. 
Copyright © 2014 Mkono Wangu Production Designed by EvMak Tanzania