CURRENT NEWS

Thursday, November 3, 2016

UN NA EU ZATOA EURO LAKI NANE KUSAIDIA WATOTO WA KIKE


Shirika la Umoja wa Mataifa la UN kwa kushirikiana na Umoja wa Ulaya (EU) wametoa Euro laki nane kuwasaidia watoto wa kike wanaoishi katika mazingira magumu na wahanga wa mimba za utotoni waishio kwenye kituo cha Faraja Young Women Development Unit .

Mwakilishi wa EU ambaye ni Afisa Miradi Anna Muro amesema kuwa msaada huo utasaidia kuwawezesha wanawake Waweze kushiriki kwenye maendeleo ya jamii .

Akizungumza katika kituo hicho kinacholelea watoto 30 wenye watoto ambao walipata mimba katika umri mdogo na kushindwa kuendelea na masomo ambapo wanasaidiwa na kituo hicho kupata elimu ya ufundi wa ushonaji na mapishi ili kupata stadi zitakaowasaidia kujikwamua kimaisha.
Mwasisi wa Shirika la Faraja Young Women Development, Martina Simon Siara akitoa maelezo kwa Maafisa wa UN na EU wakati walipotembelea kituo shirika hilo. Kutoka kushoto ni Mwakilishi wa Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini, Amon Manyama, Mwakilishi wa EU ambaye ni Afisa Miradi, Anna Muro (wa pili kulia) pamoja na Mtaalamu wa Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa (UN) nchini, Hoyce Temu (kulia).(Picha na Ferdinand Shayo).

Anna amesema kuwa watoto wengi wanakabiliwa na changamoto ya usafirishaji wa binadamu jambo ambalo ni kinyume cha haki za binadamu na haki za watoto hivyo amewataka Jamii na serikali kupiga vita usafirishwaji wa watoto.

Mwakilishi wa Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini, Amon Manyama amewataka watoto wanaoishi katika kituo hicho kutumia fursa ya mafunzo wanayoyapata kujiendeleza kielimu na kukua kiuchumi ili kutokomeza umasikini na mimba za utotoni kwa watoto wa kike.

Muasisi wa kituo hicho Martina Simon Siara ameshukuru ugeni kutoka UN na EU uliofika kituoni hapo kwa ajili ya kutazama shughuli mbalimbali zinazofanywa na kituo hicho pamoja na kuwaunga mkono ili waweze kuongeza tija katika kuisaidia jamii.
Mwakilishi wa Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini, Amon Manyama (wa pili kulia) na Mwakilishi wa EU ambaye ni Afisa Miradi, Anna Muro (wa pili kushoto) wakipata maelezo kutoka kwa Muasisi wa Shirika la Faraja Young Women Development, Martina Simon Siara (kulia) walipotembelea shirika hilo lililopo jijini Arusha.
Wawakilishi kutoka EU na UN wakitazama shughuli za mikono zinazofanywa na watoto wanaoishi katika kituo cha Faraja Young Women Development Unit walipotembelea kituo hicho hivi karibuni kilichopo jijini Arusha.
Mwakilishi wa Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini, Amon Manyama na Mwakilishi wa EU ambaye ni Afisa Miradi, Anna Muro wakishirikiana kuingiza shanga ambazo hutumika kushona mavazi ya utamaduni yanayoshonwa na watoto wa kike wanaoshi katika kituo cha Faraja Young Women Development Unit (katikati) ni mtoto mwenye ulemavu wa ngozi Rosemary Innocent.
Binti mwenye ulemavu wa ngozi, Rosemary Innocent na wenzake wakiendelea na darasa la kutengeneza vitu mbalimbali kituoni hapo.
Mwakilishi wa Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini, Amon Manyama (kushoto) na Mwakilishi wa EU ambaye ni Afisa Miradi, Anna Muro katika picha ya pamoja na binti aliyeshona vazi la kuvutia la kimasai lililonakshiwa na shanga walipotembelea kituo hicho.
Wawakilishi wa UN na EU wakitazama kitengo cha elimu ya mapishi katika Kituo cha Faraja Young Women Development Unit.
wanafunzi wanaojifunza ushonaji katika Kituo cha Faraja Young Women Development Unit.
Mwakilishi wa Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini, Amon Manyama akitazama mabinti wanaojifunza ushonaji nguo kituo cha Faraja Young Women Development Unit walipokitembelea kituo hicho kilichopo jijini Arusha.
Mtaalamu wa Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa (UN) nchini, Hoyce Temu akifafanua jambo kwa vijana na watoto wanaoishi katika kituo hicho walipokitembelea jijini Arusha.
Mwakilishi wa EU ambaye ni Afisa Miradi, Anna Muro akizungumza na wale, vijana pamoja na watoto wanaoishi kwenye kituo cha Faraja Young Women Development Unit walipokitembelea kituo hicho kilichopo jijini Arusha.
Wawakilishi wa UN na EU katika picha ya pamoja na walezi na watoto wanaoishi kwenye kituo hicho.
 
Copyright © 2014 Mkono Wangu Production Designed by EvMak Tanzania