CURRENT NEWS

Thursday, December 15, 2016

BEN POUL:NAFURAHIA MAISHA YA MUZIKI
Mwandishi Wetu

MSANII wa muziki wa kizazi kipya nchini, Ben Poul, amefurahishwa na mafanikio aliyoyapata katika onesho lake alilolifanya katika mji wa   nchini Offenbach Ujerumani, mwishoni mwa wiki iliyopita.

Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kuwasili akitokea nchini Ujerumani, Poul alisema amepata mafanikio makubwa sana katika onesho lake la nchini humo, kwa kupata mashabiki wengi ambao hakuwatarajia.

Poul alisema mafanikio hayo anaweza kusema ni makubwa hasa kwa kufanya onesho la moja kwa moja katika nchini iliyopo nje ya bara la Afrika na kupata mafanikio ya aina hiyo.

"Katika maisha yangu ya muziki ni kitu kikubwa ambacho nimeona hata wadau wangu wa muziki niwapte ujumbe kuwa nimefanikiwa na onesho langu hilo na Ujerumani na limenifanya nione kuna mwanga mkubwa kimuziki" alisema Poul.

Aidha Poul alisema  hiyo inatokana na kufanya onesho  akiwa msanii pekee yake kwa kutumia vyombo (live band) na haikuwa na waafrika ilikuwa na wajerumani na walionesha kukubali zaidi hit single yake ya ‘Moyo Mashine’.

Alisema kuwa katika onesho hilo  ilihudhuriwa na watu wanaofikia 10,000 na imeacha historia katika maisha, huku kukiwa na watanzania watatu pekee, yeye mwenyewe, Emmanuel Austin na mjomba wa Emanuel Austin.

Msanii huyo alisema katika maisha yake ya muziki onesho hilo ni la tatu kupata sapoti kubwa kutoka kwa mashabiki, ikiwa ni pamoja na onesho la Fiesta lililofanyika Dodoma kwa Wabunge wengi kupata jukwanii na onesho lingine lilikuwa usiku wa Mwafrika ambalo nalo lilikuwa na watu wengi.

"Narufahia maisha yangu ya muziki kila siku mashabiki wanakubai nanichofanya na nyimbo zangu zinapendwa kuchezwa kila kona, lakini kubwa kwangu kwenu kila mwanamuziki afurahie kazi yake haswa anapoenda sehemu kukubalika na wenyeji na sio waafrika wenzake ambao uwa wachache ni changamoto ambayo kila mmoja anatakiwa apambane nayo"alisema Poul.


Msanii huyoa anatamba na nyimbo mbalimbali ikiwemo, Sofia, Moyo Mashine, Nakuchana, Unanichora’ na hivi karibuni ameshirikishwa kwenye wimbo wa msanii Darasa ambao umeshika nafasi kubwa ya kupigwa katika vitu mbalimbali vya radio na televisheni unaitwa Muziki.
 
Copyright © 2014 Mkono Wangu Production Designed by EvMak Tanzania