CURRENT NEWS

Thursday, December 22, 2016

DC MTATURU AKIFUNGIA CHUO BUBU CHA UTABIBU

 Mkuu wa wilaya ya Ikungi, Miraji Mtaturu(aliyevaa miwani) akisikiliza   kwa makini maelezo kuhusu chuo hicho Bubu kinachotoa mafunzo   ya kitabibu kinyume na sheria.

        Wanafunzi wakiwa darasani
            ..................................................................................
Mkuu wa wilaya Ikungi, Mkoani Singida Miraji Mtaturu amefanya ziara ya kushtukiza kata ya Makilawa kijiji cha Mtavila na kutembelea  chuo kinachotoa mafunzo ya utabibu kinyume cha sheria na kuamuru kuwekwa rumande Mkuu wa Chuo Steven Fransis Mtesiwa.

Kadhalika, Mtaturu amefunga rasmi shughuli zote za chuo hicho bubu na kuagiza wanafunzi warudishiwe fedha zote walizolipa mwezi Oktoba 2016 wakati wanaanza masomo.

Kabla ya kufikia uamuzi huo, Mtaturu alifanya mahojiano na Mkuu wa chuo hicho Mtesiwa lakini alishindwa kuthibitisha uhalali wa kuendesha chuo hicho kwa mujibu wa sheria ikiwemo kuwatoza ada sh. 850,000 kwa mwaka akidai ni mchango wa wanachama wa Red cross wanaojifunza namna ya kutoa huduma ya kwanza wakati wa majanga mbalimbali.

Kufuatia hali hiyo, Mkuu wa wilaya hiyo ameamuru awekwe ndani na atoe maelezo yatakayosaidia kuujua ukweli.

Aidha Mkuu huyo ameahidi kufanya juhudi za kuwatafutia vyuo halali kwa wanafunzi wenye sifa ili waendelee na masomo.


 
Copyright © 2014 Mkono Wangu Production Designed by EvMak Tanzania