CURRENT NEWS

Saturday, December 24, 2016

KABILA KUWA MADARAKANI HADI MWAKA UJAO

Wapatanishi katika Jamhuri wa Kidemokrasia ya Congo, wameandaa mwafaka wa kuhakikisha kuwa madaraka yanapokezwa kwa njia ya amani.
Mashauriano yaliyoandaliwa na Kanisa Katoliki, yanafuatia kukataa kwa Rais Joseph Kabila, kuondoka madarakani baada ya utawala wake wa mihula miwili kukamilika.
Chini ya mapatano hayo Rais Kabila ataendelea kuwa Rais hadi wakati wa uchaguzi ifikapo mwisho wa mwaka ujao.
Waziri Mkuu mpya atachaguliwa kutoka kwa upande wa upinzani na mpango huo utasimamiwa na mkongwe wa upinzani, Etienne Tshisekedi.
Mwandishi wa habari wa BBC, alisema kuwa ingawa kuna ripoti kuwa pande kinzani zimekubaliana kwa maswala fulani, haiwezekani sahihi za mkataba huo kutiwa sahihi kabla Krismasi.
Kukataa kwa Bwana Kabila kuondoka madarakani na kuahirishwa kwa uchaguzi kumesababisha maandamano makali katika barabara kuu za miji nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
 
Copyright © 2014 Mkono Wangu Production Designed by EvMak Tanzania