CURRENT NEWS

Tuesday, December 13, 2016

KIKUNDI CHA UPENDO MLANDIZI CHASAIDIA VIFAA KITUO CHA AFYA MLANDIZI


Na Omary Mngindo, Mlandizi


KIKUNDI cha Wamama Upendo kilichopo Mlandizi Kibaha Vijijini Mkoawa Pwani Maarufu Mama Mlezi wa Familia kimekabidhi vifaa tiba katika Kituo cha afya cha Mlandizi kilichopo mjini hapa.
Wakiongozwa na Mwenyekiti wa kikundi Frida Gongi, Katibu Tanibu Mshindo na Mhazin Consorata Swai, msafara huo pia umepata baraka kutoka kwa Mwenyekiti Mwinyimvua Pazi wa Kitongoji cha Mihande na Ally Nyambwilo wa Mlandizi Kati   abapo msafara wa wanakikundi hao 50 walifika kwenye Kituo hicho kwa lengo la kukabidhi vifaa tiba ambavyo ni pamoja na kugawa sabuni za kukogea na kufulia, dawa za meno, mafuta ya kupaka ya mgando na maji.
Mbali ya vitu hivyo kwa wagonjwa ambao walikuwa wamelazwa wodini, pia wamekabidhi vifaa tiba ambavyo ni pamoja na vikinga mikono (Grops) boks 10 vifaa vya kuchomea sindano boksi moja lenye vifaa vya kuchomea sindano vipatavyo 200 na sabuni ya maji lita 10 kwa ajili ya kusafishia sakafu vyote vikiwa na thamani ya sh. Laki 3.
Taarifa ya kikundi iliyosomwa na Katibu Tanibu imeeleza kuwa kikundi chao chenye wanachama 50 jinsia ya kike pekee kimeanzishwa mwanzoni mwa mwaka 2016 ambapo wanakutana mara moja kwa mwezi kwa kuchangia sh. 2,000 kila mmoja, wamenunua vifaa mbalimbali vya kupikia pamoja na viti ambapo wanakodisha kwenye shughuli tofauti, na kwamba wameamua kufika kwenye kituo hicho kuwapatia faida kidogo ambayo wameipata.
“Tunatanguliza shukrani zetu za dhati kwa kupata kibali cha kufika hapa kwenye kituo chetu cha afya cha Mlandizi tumekuja kukabidhi kwa Mganga wa kituo hivi vitu kidogo vya tiba ambavyo sisi kikundi chetu Mwenyezimungu ametujaalia, hii ni moja ya mahudhui kwetu, Kaulimbiu yetu inasema Mama ni Mlezi wa Famili,” alimalizia hivyo.
Kwa upande wake Mwenyeviti wa Kitongoji cha Mihande Mwinyimvua Pazi na Mlandizi Kati Ally Nyambwilo kila mmoja alikuwa na neon la kuzungumza na kikundi hicho ambapo Mwinyimvua ambaye pia alimwakilisha mgeni rasmi Diwani wa Kata hiyo Ephrasia Kadala alisema kuwa amefurahishwa na moyo huo ambao umeoneshwa na akina mama hao huku aisema kuna vikundi vingi vyenye uwwezo lakini hawajajaaliwa kuwa na moyo kama huo.
Nyambwilo aliwashukuru huku akiwataka tukio hilo liwe mwanzo kwao katika kujitoa katika jamii na kwamba kuna maeneo mengi yanahitaji pa misaada hivyo kikundi hicho kiwe mwanzo kwao kujitokeza katika kujikita kutoa misaa kwa jamii hizo.
MWISHO.
 
Copyright © 2014 Mkono Wangu Production Designed by EvMak Tanzania