CURRENT NEWS

Wednesday, December 21, 2016

KWAYA YA VIJANA KKKT IRINGA NA MWIMBAJI MWASONGWE KUFUNIKA TAMASHA YA UIMBAJI MAFINGA, KIPANGULA KUWA MGENI RASMI

Image result for ambwene Mwasongwe
Mwimbaji Ambwene  Mwasongwe
WAKATI siku  za tamasha  kubwa la  kihistoria mjini Mafinga  mkoani Iringa zimezidi  kusogea  ,mkuu  wa   jimbo la kanisa la  Kiinjili la Kilutheri Tanzania  (KKKT) jimbo la Mafinga  mchungaji Antony Kipangula ndie atakayezindua tamasha   hilo .

Image result for Kwaya  ya vijana KKKT Iringa
Kwaya  ya  vijana KKKT usharika wa Iringa mjini siku ilipotembelea  bungeni Dodoma
Akizungumza leo  na mwandishi wa habari hizi ,Mratibu  wa  tamasha   hilo Mary  Mungai  aliyesa   kuwa uzinduzi  wa  tamasha  hilo utakwenda  sambamba na uzinduzi  wa  ukumbi wa  kisasa KWA  AJILI ya burudani na shughuli mbali mbali  ukumbi wa MAM ulipo katikati ya mji wa Mafinga  na  kuwa  washindi  wa uimbaji KKKT nchini  kwaya ya vijana   usharika  wa kanisa  kuu Iringa na mwimbaji wa nyimbo za injili maarufu nchini Ambwene Mwasongwe  wataongoza kupamba tamasha  hilo pamoja na kwaya  nyingine na  waimbaji binafsi kutoka  ndani na nje ya Mafinga .
"  kutakuwa na  waimbaji  wengine mbali mbali pamoja na burudani nyingine na  kuwa  lengo  la tamasha  hilo  pamoja na kutoa  burudani kwa  wakazi wa wilaya ya Mufindi na mikoa ya Iringa  na Njombe  bado itakuwa ni  siku ya  uzinduzi wa   ukumbi wa  burudani na sherehe mbali mbali katika mji huo wa Mafinga"

Mungai alisema  kuwa  kwa ajili ya  kuwashukuru  wananchi wa mji  wa Mafinga  kwa ushirikiano mbali mbali ambao  wameendelea  kuutoa amelazimika  kuandaa tamasha hilo ambalo  wananchi  watashuhudia  kwa  kiingilio kidogo  sana  kama  sehemu ya kuchangia  gharama ndogo ndogo  za  maandalizi ya  tamasha  na mchango kwa  V.I.P  utakuwa ni Tsh 10,000  wakati kawaida kwa  watu  wazima ni Tsh 5000 na watoto ni Tsh 3000 pekee  na  kuwa  ili  kuepusha  msongamano mlangoni tiketi  tayari zinauzwa katika  ofisi ya  shule ya Southern Highlands Mafinga , Hazina Bima na  Stationary ya Huruma Msigala na getini pia  zitauzwa .

Alisema   pamoja na  kuwa  wilaya ya  Mufindi  ni moja kati ya  wilaya  zenye  uchumi  mkubwa  hapa nchini na  watu  wake  ni  wale  wanaopenda burudani  mbali  mbali  zikiwemo  za matamasha ya  nyimbo  za  injili  ila bado kumbi nyingi zilizokuwepo haziwezi  kukidhi mahitaji ya burudani  na kuwa  kuzinduliwa  kwa  ukumbi huo  kutafungua  milango ya  uchumi kwa  mji   huo kwa    wadau kutoka ndani ya wilaya ya  Mufindi na nje ya  mkoa kufika  kuutumia ukumbi huo kuandaa burudani mbali mbali na hata  kuutumia kwa mikutano mikubwa . 


Mwenyekiti wa  kwaya  ya  vijana usharika wa kanisa  kuu Kombo Mdegella akizungumzia juu ya maandalizi ya ushiriki  wao katika  tamasha  hilo  alisema  kwaya yake  ambayo  imekuwa  ikifanya  vema  katika mashindano mbali mbali ya  uimbaji ipo  kwenye maandalizi makubwa ya  kuhakikisha wanatoa burudani ya nyimbo  kali  kwenye Tamasha   hilo .

 ukumbi pekee katika mikoa ya nyanda za  juu kusini kujengwa  kisasa na utakuwa na majukwaa mawili  moja la kati  litakuwa ni  jukwaa  linalotembea pia  kutakuwa na V.I.P kwa wageni maalum ambao ili  waweze  kuingia ukumbini watapandishwa ghorofani  kwa ngazi maalum   na  kushuka kwa  ngazi hadi  jukwaani iwapo watataka  kutoingilia mlango wa waalikwa  wote .
 
Copyright © 2014 Mkono Wangu Production Designed by EvMak Tanzania