CURRENT NEWS

Friday, December 9, 2016

MBUNGE WA CHALINZE RIDHIWANI AKAGUA SHUGHULI ZA MAENDELEO JIMBONI


      
Mbunge wa jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete akizungumza na wananchi wa Kibindu baada ya kumaliza ziara ya siku moja ya kukagua maendeleo na kuzungumza na wananchi.


                 Wananchi wakimsikiliza Mbunge wao, Ridhiwani Kikwete.
   
    wananchi wa Kibindu wakimsikiliza Mbunge wao wa jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete.

                    ................................ .......................................................................................

Mbunge wa jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete ameanza ziara yake ya kukagua maendeleo na kuzungumza na wananchi wa jimbo lake huku akiwashukuru kwa ushirikiano wanaoutoa kufanikisha maendeleo ya jimbo la Chalinze.

Akizungumza na  wananchi katika vijijini vya Kwakonje,kibindu na kwa msanja,Mbunge huyo amewashukuru wananchi kwa ushirikiano wao ambao umewezesha kufanikisha shughuli za kimaendeleo  kwa wakati.

Ziara ya mbunge inaendelea leo katika kijiji cha msolwa, mboga, na lugoba ambapo atakagua maendeleo ya ukamilishaji wa hospitali ya Msoga,ujenzi wa zahanati ya wakina mama kiwangwa, ujenzi wa mabweni moleto na mboga sekondari, nyumba za walimu moleto sekondari akiwa na kauli mbiu mbunge yupo kazini.
 
Copyright © 2014 Mkono Wangu Production Designed by EvMak Tanzania