CURRENT NEWS

Saturday, December 17, 2016

MPOGOLO ATINGA MAKAO MAKUU YA CCM MJINI DODOMA LEO, LUHWAVI AMKABIDHI OFISI

Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara, Rodrick Mpogolo akikaribishwa na Katibu wa Sekretarieti, Anamringi Macha, alipowasili leo jioni Makao Makuu ya CCM, mjini Dodoma kukabidhiwa rasmi Ofisi na aliyekuwa Katibu Mkuu Mstaafu wa CCM-Bara, Rajab Ruhwavi.
Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara, Rodrick Mpogolo akikaribishwa na Naibu Katibu Mkuu Mstaafu wa CCM-Bara, Rajab Luhwavi alipowasili Makao Makuu ya CCM mjini Dodoma leo jioni kwa ajili ya Luhwavi kumkabidhi Ofisini. Katikati ni Katibu wa Sekretarieti, Anamringi Macha.Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara, Rodrick Mpogolo (watatu kushoto), akifuatana na viongozi waandamizi wa CCM, kwenda ukumbini kwenye mazungumzo baada ya kuwasili Makao Makuu ya CCM mjini Dodoma leo jioni kukabidhiwa ofisini. Kushoto ni Katibu wa Sekretarieti, Anamringi Macha, na wapili ni Katibu Mkuu Mstaafu wa CCM-Bara, Rajab Ruhwavi
Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara Rodrick Mpogolo (kushoto) na Naibu Katibu Mkuu Mstaafu wa CCM-Bara, Rajabu Luhwavi, wakisalimia Makatibu Muhtasi wa Ofisi ya Katibu Mkuu wa CCM na Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara, walipoingia katika ofisi ya Makatibu Muhtasi hayo kabla ya Mpogolo kufanya kikao na viongozi waandamizi wa Makao Makuu hayo ya CCM. Kushoto ni Evalida Mafuta na Elizabeth Mhina.
 Mpogolo na Luhwavi wakiwasili ukumbini kuzungumza na viongozi waandamizi wa Makao Makuu ya CCM.
 Mpogolo akisaini Kitabu cha wageni kabla ya mazungumzokuanza. Kulia ni Luhwavi


Katibu wa Sekretarieti ya CCM, Anamringi Macha akikaribisha ugeni kabla ya mazungumzo ya Mpogolo na watumishi waandamizi wa Makao Makuu ya CCM mjini Dodoma
 Viongizi wakiwa tayari kwa kikao hicho na Mpogolo 

Naibu Katibu Mkuu mstaafu wa CCM-Bara, Rajab Luhwavi akizungumza kabla ya kumkaribisha Mpogolo kuzungumza

Naibu Katibu Mkuu Mstaafu wa CCM, Rajab Luhwavi akimkaribisha kuzungumza, Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara, Rodrick Mpogolo 
Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara, Rodrick Mpogolo akizungumza na viongozi waandamizi wa Makao Makuu ya CCM mjini Dodoma leo. katika mazungumzo hayo Mpogolo amewataka viongozi hao kumpa ushirikiano ili kuongoza vizuri, huku akisisitiza kuwa atakuwa akifanyakazi kwa kufuata mstari ulionyooka,na pale atakapokuwa akilazimika kusema hatakuwa akimung'unya maneno. Kulia ni Luhwavi. 
Katibu Msaidizi Mkuu katika Idara ya Utawala Ndigu Mdaki akitoa shukrani kwa Mwenyekiti wa CCM, Rais John Magufuli kuwaletea CCM Mpogolo.
Katibu Msaidizi Ndugu, Kazidi naye akitoa shukrani na maneno machache baada ya kupewa nafasi ya kuzungumza mwishoni mwa mazungumzo hayo
Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara Rodrick Mpogolo (watatu kushoto-walioketi) na Naibu Katibu Mkuu Mstaafu wa CCM-Bara, Rajab Luhwavi wakiwa katika picha ya kumbukumbu na viongozi hao waandamizi wa makao makuu ya CCM mwishoni mwa mazungumzo
Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara Mpogolo na Naibu Katibu Mkuu Mstaafu wa CCM-Bara, Luhwavi wakiwa kakatika Ofisi ya Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara, tayari kwa makabidhiano ya ofisi hiyo huku viongozi waandamizi wa Makao makuu ya CCM wakishuhudia.PICHA ZOTE NA BASHIR NKOROMO-theNkoromo Blog 
 
Copyright © 2014 Mkono Wangu Production Designed by EvMak Tanzania