CURRENT NEWS

Sunday, December 25, 2016

SALAMU ZA SIKUKUU YA CHRISTMAS KWA WANANCHI WA MKOA WA DAR ES SALAAM


Ndugu wana Dar es Salaam,

Kwa niaba ya serikali ya Mkoa wetu, napenda kuchukua fursa hii kwa dhati kabisa kuwatakia waumini wote wa kikristo na wana Dar es salaam kwa ujumla sikukuu njema ya Christmas yenye furaha, upendo, amani na utulivu.

Ni muhimu wana familia kuchukua tahadhari za kiusalama katika siku hii ikiwemo kuongeza umakini na uangalizi wa watoto maeneo ya fukwe (beach) ili kuondoa uwezekano wa maafa, kutoondoka nyumbani bila kuacha angalau mtu mmoja mzima wa kubaki kutazama usalama wa nyumba na kuzidisha umakini katika matumizi ya barabara.

Tusisite kutoa taarifa kwa jeshi letu la polisi pindi tunapoona viashiria vya uhalifu au kuvunjika amani katika maeneo tuliyopo.

Nawasihi tutumie siku hii kuiombea nchi yetu iendelee kuwa ya amani na utulivu, na tuwaombee viongozi wetu akiwemo Rais wetu mpendwa Dr. John Pombe Joseph Magufuli na wasaidizi wake wote ili waendelee kuitumikia nchi yetu vema.
Aidha tuwajali wagonjwa, walemavu, yatima na watu wasiojiweza katika maeneo yetu tunayoishi ili nao waweze kusherehekea siku hii kwa furaha.

Mwisho nawatakia heri, furaha na amani katika sikukuu hii ya Christmas.

ALLY HAPI
KAIMU MKUU WA MKOA
DAR ES SALAAM
 
Copyright © 2014 Mkono Wangu Production Designed by EvMak Tanzania