CURRENT NEWS

Thursday, December 22, 2016

TANROADS KUONDOA KERO YA UKOSEFU WA MITARO MLANDIZI

Madimbwi ya maji yaliyotuama maji ya mvua na mlundiko wa uchafu kando ya barabara kuu, eneo la Mlandizi,yakionekana pichani,ambayo ni kero ya miaka mingi hivyo mbunge wa jimbo la Kibaha Vijijini Hamoud Jumaa kulazimika kusimamia kero hiyo kwa wakala wa barabara Tanroads(Picha na Mwamvua Mwinyi)

 Mkaguzi wa barabara kutoka wakala wa barabara( Tanroads) mkoani Pwani, Livingstone Urio ,akitolea ufafanuzi jambo,kwa mbunge wa jimbo la Kibaha Vijijini ,Hamoud Jumaa mwenye kofia pama,mara baada ya kutembelea barabara kuu eneo la Mlandizi ili kuanza kwa matengenezo ya mitaro kando mwa barabara hiyo.(picha na Mwamvua Mwinyi)

 Mkaguzi wa barabara kutoka wakala wa barabara( Tanroads )Mkoani Pwani,Livingstone Urio wa katikati akikagua barabara kuu  ya Dar es salaam- Morogoro eneo la  Mlandizi ,ili kuanza kwa matengenezo ya mitaro kando mwa barabara,wa kushoto ni mbunge wa jimbo la Kibaha Vijijini,Hamoud Jumaa.(picha na Mwamvua Mwinyi)Na Mwamvua Mwinyi,Kibaha Vijijini
WAKALA wa barabara (TANROADS)mkoani Pwani ,unatarajia kufanya marekebisho na kuchimba mitaro kandokando ya barabara kuu ya Morogoro-Dar es salaam eneo Mlandizi katika kipindi cha mwaka 2016-2017.
Matengenezo hayo yatawezesha kuondoa kero kubwa iliyopo sasa ya kutuama kwa maji ya mvua na kusababisha uchafu na mazingira hatarishi kwa jamii.
Aidha wakala huo umejipanga kutumia meno ya sheria zake ,kwa kuanza kuwapiga faini ya 300,000 ama kwenda jela ,wananchi wanaweka majalala  na kutupa taka kando ya hifadhi ya barabara.
Mkaguzi wa barabara kutoka TANROADS Pwani,Livingstone Urio,aliyasema hayo baada ya kuitika wito kutoka kwa mbunge wa jimbo la Kibaha Vijijini Hamoud Jumaa,aliyewaomba watoke ofisini kwenda kujionea hali halisi.
Alisema wamejionea hali iliyopo na uchafu wa mazingira unaosababishwa na madimbwi ya maji machafu yanayotokana na kutuama kwa maji ya mvua.
Urio alieleza kwamba jukumu lao kwa sasa ni kufanya matengenezo ambapo mpango huo utatekelezwa ndani ya mwaka huu wa fedha.

“Tumeitika wito wa mbunge Jumaa ambae alifikishiwa malalamiko haya kutoka kwa wanaanchi wakati wa ziara yake na sasa yupo kwenye utekelezaji,.Alitupigia simu na kuhitaji tuje kujionea uharibifu uliopo na kero kwa jamii”

“Tatizo kubwa sura hii ipo mjini kabisa kwenye barabara kuu sasa,tumefika kumweleza pia kuwa tunatambua hili,na lipo kwenye mpango na wahakikishia wananchi kuwa tutatatua suala hili “alisema Urio.
Urio alisema ameambatana na injinia Christina Nyamzige ,hivyo anaamini wataalamu wenzake watashirikiana kuondoa changamoto hiyo .

Hata hivyo akizungumzia kuhusiana na zoezi la kutoza faini kwa wale wanaokiuka sheria zao zinazodhibiti uchafu kando ya barabara na kupaki magari alisema,sheria inawataka kuwalipisha watu hao 300,000 au kwenda jela.

Urio alifafanua kuwa uchafu unaolundikwa na kutuama kwa maji kunasababishwa na huduma za kijamii ambayo ni changamoto kubwa na wanapambana nayo katika maeneo mengi ya mkoa na nchi kijumla.
“Tutasimamia sheria hizi ili iwe fundisho kwani hairuhusiwi kupaki wala kuendesha gari kando ya hifadhi ya barabara,kutupa takataka,kulima na kupelekea mabega ya barabara kuharibika ama kuweka mashimo’alisisitiza.
Alieleza kwasasa wanashiriiana na watendaji na wenyeviti wa vijiji na vitongoji huku wakifanya mikutano ya wananchi kutoa elimu juu ya kuepukana na vyanzo vya uharibifu wa miundombinu hiyo.
Nae mbunge wa jimbo hilo,Hamoud Jumaa,alishukuru kuitikiwa wito na wakala huo kwani wameonyesha ujali na kuwa nae pamoja kukabiliana na changamoto hiyo.
Alisema hayo ni matokeo ya ziara yake ya siku 30 aliyoifanya jimboni hapo,ambapo alifikishiwa kero hiyo kutoka kwa wananchi.

Jumaa alisema tatizo kubwa ni madimbwi mengi kando ya barabara hivyo kuamua kuwakabili TANROADS kusimamia suala hilo.

Alisema atahakikisha miundombinu ya barabara inatengenezwa ili kurejesha sura nzuri ya Mji wa Mlandizi ambao upo usoni mwa barabara kuu.
Mbunge huyo alisema suluhisho la maji kuacha kutuama na kuweka madimbwi ni kupeleka maji bondeni ili yasisimame na kupelekea uchafu hatarishi.
Jumaa alisema wananchi waache kugharimu serikali kwa kufanya huduma za kijamii zinazoharibu mazingira,waache kuharibu barabara na kuweka majalala kando ya barabara hizo.
Mwenyekiti wa serikali ya kitongoji cha Mlandizi Kati ,Ally Nyambwilo na diwani wa kata ya Mlandizi Kadala,walimshukuru walimshukuru mbunge Jumaa kwa kupokea kero hiyo na Tanroads kusimamia tatizo hilo.
 
Copyright © 2014 Mkono Wangu Production Designed by EvMak Tanzania