CURRENT NEWS

Wednesday, December 7, 2016

TPA YAPOKEA MSAADA WA DOLA ZA MAREKANI MILIONI 60 KWA AJILI YA MIRADI YA BANDARI

 Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Eng. Deusdedit Kakoko (watatu kulia) na Mkurugenzi Mkazi wa TradeMark East Africa (TMEA), Bw. John Ulanga (wapili kulia) wakiweka saini makubaliano hayo mbele ya vyombo vya habari
 Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Eng. Deusdedit Kakoko akibadilishana hati ya makubaliano na Mkurugenzi Mkazi wa TradeMark East Africa (TMEA), Bw. John Ulanga mara baada ya kuweka saini makubaliano hayo.
 Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Eng. Deusdedit Kakoko na Mkurugenzi Mkazi wa TradeMark East Africa (TMEA), Bw. John Ulanga wakionesha hati ya makubaliano mara baada ya kuweka saini makubaliano hayo.
Baadhi ya Waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari wakishuhudua tukio hilo.
 Mkuu wa Shirika la DFID Tanzania, Bw. Vel Gnanendran akizungumza na waandishi wa habari katika hafla hiyo. Katikati ni Kaimu Naibu Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Eng. Karim Mattaka.
 Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Eng. Deusdedit Kakoko (wanne kushoto) akijibu maswali ya waandishi wa habari katika hafla hiyo.
Mkurugenzi Mkazi wa TradeMark East Africa (TMEA), Bw. John Ulanga (kulia) akijibu maswali ya waandishi wa habari katika hafla hiyo.
Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) leo imeingia makubaliano na Kampuni ya TradeMark East Africa (TMEA) ambayo itatoa msaada wenye thamani ya Dola Marekani Milioni 60 sawa na Shilingi za Kitanzania Bilioni 132 kwa ajili ya maboresho ya miradi mbalimbali ya Bandari ya Dar es Salaam.
Msaada huo unatarajiwa kusaidia uboreshaji wa barabara za ndani ya bandari, eneo la uhifadhi wa makontena, mizigo, kuongeza uwezo wa bandari kuchukua meli kubwa zaidi, kuendesha upembuzi yakinifu wa kuanisha maeneo mengine ya maboresho, kuifanya bandari ya dar es salaam kuwa rafiki ‘green port’ na kuangalia maboresho zaidi ya mifumo ya kielektroniki.
Makubaliano hayo yamefanyika leo Makao Makuu ya Mamlaka ambapo Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Eng. Deusdedit Kakoko na Mkurugenzi Mkazi wa TradeMark East Africa (TMEA), Bw. John Ulanga walitia saini makubaliano hayo mbele ya vyombo vya habari.
 
Copyright © 2014 Mkono Wangu Production Designed by EvMak Tanzania