CURRENT NEWS

Tuesday, December 20, 2016

WANAFAMILIA WA ABC DENTAL CENTRE YAGAWA MISAADA KWA WATOTO WENYE MAHITAJI MAALUM WA KITUO CHA KIND HEART AFRICA CHA CHANIKA DAR ES SALAM


 Wanafamilia wa ABC Dental Centre inayomiliki na kuendesha ABC Dental Clinic wakiwa katika picha ya pamoja mara walipofika katika Kituo cha kulelea watoto wenye mahitaji Maalum kilichopo Chanika

 Mmoja wa wanafamilia Hassan akishusha vitu walivyoviandaa kwa ajili ya misaada ya watoto wenye mahitaki maalum kwa lengo la kuwawezesha watoto hao kufurahia na kujumuika na waumini wote Duniani katika  kusherehekea Sikukuu za Krismas na Mwaka Mpya kwa furaha Wanafamilia hao wakijumuika na watoto hao kuiba wimbo kwa pamoja wa kuwakaribisha wageni


 Mkurugenzi na Mlezi wa  ABC Dental Centre inayo miliki na kuendesha ABC Dental Centre, Happy Kidata (wa tatu kulia) akimkabidhi Mratibu wa Kituo hicho, Teddy Kimatare misaada mbalimbali yenye thamani ya zaidi ya Sh. Milioni moja ikiwa ni kuadhimisha mwaka Mmoja  tangu kuanzishwa ABC Nov, 2015, , wanafamilia wa ABC Dental Centre pamoja na marafiki na wadau wamshukuru Mungu kwa kutowa Sadaka kwa kuwatembelea watoto wenye mahitaji Maalum  kwa kuwawezesha kwa kusherehekea Sikukuu za Krismas na Mwaka Mpya kwa furaha

 Mkurugenzi wa ABC Dental Clinic, Dokta. Gombo Felician (wa nne kulia) akisaidiana na  Mkurugenzi na Mlezi wa  ABC Dental Centre inayo miliki na kuendesha ABC Dental Centre, Happy Kidata (wa tatu kulia) kumkabidhi, Mratibu wa Kituo hicho, Teddy Kimatare ndoo ya mafuta ya kula na alisema Dokta Gombo,  Tumekuja kuwatembelea kwa kuwaletea zawadi kigo kwa kuwaonyesha upendo kama tupo pamoja nanyi, tumewaletea zawadi kwa ajili ya Sikukuu na zawadi hizo ni viatu vya watoto wa kike na wakiume, kunanguo za watoto wa kike na watoto wa kiume, madaftari mengi, kalamu za wino na penseli nyingi, mashuka mazuri kwa ajili ya vitanda vyenu kwa watoto wa kike na watoto wa kikiume , sabuni zenye dawa za kuogea za kuzuia upere na sabuni za kufulia pamoja na  nguo za watoto wakike na za wavulana na pia tumewaletea Sukari na mafuta ya kula
   Mkurugenzi na Mlezi wa  ABC Dental Centre inayo miliki na kuendesha ABC Dental Centre, Happy Kidata (wa tatu kulia)  akikadhidhi mfuko wa Sukari kwa watoto hao pamoja na Mratibu wa Kituo hicho, Teddy Kimatare, (aliyevaa kitenge )
 
(PICHA ZOTE NA KHAMISI MUSSA) Mmiliki wa Kampuni ya KM Express Photo Studio na Mmiliki wa ujijirahaa blog
 
Copyright © 2014 Mkono Wangu Production Designed by EvMak Tanzania