CURRENT NEWS

Saturday, January 28, 2017

CCM ZANZIBAR YAZINDUA SHEREHE ZA KUADHIMISHA MIAKA 40

Naibu Kaitibu Mkuu Chama Cha Mapinduzi,Zanzibar Ali Vuai Ali wa pili kutoka kushoto akiwa na wana CCM katika uzinduzi wa sherehe za miaka 40 za chama hicho kwa kufanya usafi.

 Naibu Kaitibu Mkuu Chama Cha Mapinduzi,Zanzibar Ali Vuai Ali wa pili kutoka kulia akiwa na wana CCM katika uzinduzi wa sherehe za miaka 40 za chama hicho kwa kufanya usafi.
Naibu Kaitibu Mkuu Chama Cha Mapinduzi,Zanzibar Ali Vuai Ali  katika uzinduzi wa sherehe za miaka 40 za chama hicho kwa kufanya usafi.     Chama cha Mapinduzi ccm mapema leo kimzidua   sherehe  cha kuadhimisha miaka 40 tangu kuzaliwa chama hicho kwa ufanyaji usafi katika maeneo ya soko la darajani katika Wilaya ya mjini.
     Akizungumza na wanachama wa chama hicho katika hafla ya shughuli za usafi Naibu katibu Mkuu wa chama hicho Vuai  Ali Vuai amesema  nijambo la kujivunia  kwa chama cha mapinduzi ccm kutimiza miaka 40  tokea kuzaliwa kwake ambapo  hatua mbali mbali za maendeleo zimepatikana  ikiwemo huduma za Afya,Elimu,huduma za maji safi na salama,pamoja na kukabiliana na suala  zima la ajira kwa vijana.
      Hata hivyo amesema lengo la  kuundwa chama cha mapinduzi  ni kuendeleza  harakati zilizokuwa zikifanywa na vyama vya ASP na TANU za kuwaletea maendeleo  Watanzania kwa haraka bila ya ubaguzi  wa aina yoyote nchini kwani ndivyo vyama zilivyoleta ukombozi.
     Kwaupande wao baadhi ya Viongozi wa ccm katika ngazi mbalimbali za chama  wametoa wito kwa vijana wote nchini  kukiunga mkono chama cha mapinduzi  ambacho   kilifanya ukombozi  kutoka kwa masultani  kwa lengo la kuwapatia uhuru watanzania  ili kulinda  amani  na upendo.
       Aidha wamesema vijana  wanamchango mkubwa  katika chama, hivyo elimu kwa vijana hao inahitajika kwani baadhi yao wamekuwa na wigo na kukizarau chama na kukiona hakina faida jambo ambalo inakipa wakati mgumu chama hivyo katika kufikia hatua zake  zinazokusudia.
       Kilele cha  sherehe hizo  za kutimiza miaka 40 ya chama cha mapinduzi zinatarajiwa kuadhimishiwa Dodoma siku ya tarehe 5 ambapo  zitaadhimishwa kwa mikutano ya ndani  na  makongamano na kwani mikutano ya hadhara  imedhuiliwa na kwa Zanzibar  wataadhimisha kwa  kufanya michezo mbalimbali.
 
Copyright © 2014 Mkono Wangu Production Designed by EvMak Tanzania