CURRENT NEWS

Tuesday, January 17, 2017

MTOTO WA RAIS MTEULE WA GAMBIA ADAMA BARROW AFARIKI BAADA YA KUUMWA NA MBWA


Mtoto wa kiume wa rais mteule wa Gambia Adama Barrow amefariki baada ya kuumwa na mbwa.
Habibou Barrow alifariki alipokuwa akipelekwa hospitalini kufuatia kisa hicho cha siku ya Jumapili, kilichotokea eneo la Manjai karibu na mji mkuu Banjul.
Mazishi yake tayari yashafanyika.
Bwana Barrow yuko nchini Senegal kabla ya kuapishwa siku ya Alhamisi.
Kwa mjibu wa ripoti hiyo, Barrow ana wake wawili na watoto wengine wanne
 
Copyright © 2014 Mkono Wangu Production Designed by EvMak Tanzania