CURRENT NEWS

Sunday, January 15, 2017

MWANDISHI WA GAZETI LA UHURU AMINA ATHUMAN AFARIKI DUNIA

Marahemu Amina Athuman enzi za uhai wake akiwa katika Sherehe za Mapinduzi uwanja wa Amaan Zanzibar.

UONGOZI wa Kampuni ya Uhuru Publications Ltd, inayochapisha magazeti ya Uhuru, Uhuru Wikiendi, Burudani na Mzalendo, unayo masikitiko makubwa kutangaza kifo cha mwandishi wake Amina Athumani.

Amina, mwandishi wa habari za michez katika magazeti hayo, amefariki leo asubuhi katika Hospitali ya Mnazi Mmoja mjini Unguja, alikokuwa amelazwa.

Amina, alilazwa kwenye hospitali hiyo baada ya kuzidiwa kutokana na kushikwa uchungu, ambapo alijifungua mtoto wa kiume, lakini kwa bahati mbaya alifariki.

Baada ya mtoto kufariki, Amina aliendelea kupatiwa matibabu hadi mauti yalipomkumba leo asubuhi.

Marehemu Amina alikwenda Zanzibar kikazi kwa ajili ya kuripoti mashindano ya Kombe la Mapinduzi, yaliyomalizika Ijumaa iliyopita. Ilikuwa arejee Dar es Salaam jana.

Mipango inafanywa na ofisi kwa ajili ya kuurejesha mwili wake Dar es Salaam leo jioni kwa boti na msiba upo nyumbani kwa ndugu wa marehemu, Kariakoo.

Mungu ailaze roho ya marehemu Amina Athumani mahala pema.

Copyright © 2014 Mkono Wangu Production Designed by EvMak Tanzania