CURRENT NEWS

Thursday, January 19, 2017

TIB KUSAIDIA UJENZI WA KIWANDA CHA VIFAA VYA HOSPITALI SIMIYUBenki ya Maendeleo ya TIB imesema tayari iko katika mchakato wa kutoa mkopo wa ujenzi wa kiwanda kitakachozalisha vifaa vyote vya hospitali vitokanavyo na mazao ya pamba hapa nchini badala ya kuviagiza vifaa hivyo kutoka nje ya nchi.

Mkurugenzi Mkuu wa TIB Development Be Charles Singili, ameiambia Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Simiyu kuwa tayari Benki imeshapata ukubali wa kutoa mkopo huo.

Bw Singili alisema Mkoa wa Simiyu una uwezo na faida ya kiushindani (competitive advantage) ya kujenga viwanda vitakavyo zalisha vifaa vya hospitalini vinavyotokana na mazao ya pamba.

Benki hiyo pia imekubali kutoa fedha kuimarisha Kiwanda cha chaki ili kuongeza uwezo wa uzalishaji kukidhi mahitaji ya nchi nzima.

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mh Anthony Mtaka na Katibu Tawala wake (RAS) Jumanne Sagini, wameishukuru sana TIB kwa kukubali kuunga mkono juhudi za wanasimiyu katika kutafsiri dhamira ya Mh Rais Magufuli ya kujenga Tanzania ya Viwanda.

"Tunata Mh Rais akija tena kututembelea Simiyu, aone anachokidhamiria", alisema.

Tunashukuru sana kwa ukubali wenu kuwa washirika muhimu kutuunga mkono katika azma yetu ya kuigeuza Simiyu kuwa kanda maalum ya kiuchumi.
 
Copyright © 2014 Mkono Wangu Production Designed by EvMak Tanzania