CURRENT NEWS

Monday, January 16, 2017

WAZIRI MKUU AZINDUA SAFARI ZA ATCL DAR/DODOMA

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipokea mfano wa Boarding Pass kutoka kwa Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mahandisi Edwin Ngonyani kabla ya kusafiri kwa ndege ya Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) kutoka uwanja wa ndege wa Julius Kambarage Nyerere, Dar es salaam kwenda Dodoma Januari 16, 2017. Alikuwa akizindua safari za ndege za shirika hilo kati ya viwanja viwili hivyo.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na wafanyakazi wa Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) kabla ya kupanda ndege ya Shirika hilo kwenye uwanja wa Ngege wa Julius Kambarage Nyerere kwenda Dodoma ikiwa ni uzinduzi wa safari za ndege za ATCL kati ya viwanja viwili hivyo, Januari 16, 2017.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisafiri kwa ndege ya Bombardier Q400 ya Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) kutoka uwanja wa ndege wa Julius Kambarage Nyerere kwenda Dodoma Januari 16, 2017. Alikuwa akizindua safari za ndege za ATCL katika viwanja viwili hivyo. Kushoto kwake ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Leonard Chamuriho.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwapungia viongozi na wananchi wa Dodoma baada ya kutua kwenye uwanja wa ndege wa Dodoma akitoka uwanja wa ndege wa Julius Kambarage Nyerere jijini Dar es salaam Januari 16, 2017 ikiwa ni uzinduzi wa Safari za ndege za Shirika hilo kati ya viwanja viwili hivi.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Watu Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Dodoma akitoka uwanja wa ndege wa Julius Kambarage Nyerere jijini Dar es salaam ikiwa ni uzinduzi wa safari za ndege za Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) Januari 16, 2016.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Jordan Rugimbana ​ baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Dodoma akitoka uwanja wa ndege wa Julius Kambarage Nyerere jijini Dar es salaam ikiwa ni uzinduzi wa safari za ndege za Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) kati ya viwanja viwili hivyo, Januari 16, 2016. Wapili kushoto ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijan, Ajira na Watu Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mtendaji Mkuu wa Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL), Kapteni Richard Shaidi baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Dodoma akitoka uwanja wa ndege wa Julius Kambarage Nyerere jijini Dar es salaam ikiwa ni uzinduzi wa safari za ATCL kati ya viwanja viwili hivyo, Januari 16, 2017. Kulia kwake ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Leonard Chamuriho. Wapili kushoto ni Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Anthony Mavunde na kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Dodoma, Christina Mndeme.


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na wafanyakazi wa Shirika la Ngege ya Tanzania (ATCL) baada ya kutua kwenye uwanja wa ndege wa Dodoma akitoka uwanja wa ndege wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam ikiwa ni uzinduzi wa safari za ndege za ATCL kati aya viwanja viwili hivyo, Januari 16, 2017.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Waziri Mkuu Mstaafu, John Malecela baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Dodoma akitoka uwanja wa ndege wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam ikiwa ni uzinduzi wa safari za ndege za ATCL kati aya viwanja viwili hivyo, Januari 16, 2017.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Spika wa Bunge, Job Ndugai baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Dodoma akitoka uwanja wa ndege wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam ikiwa ni uzinduzi wa safari za ndege za ATCL kati aya viwanja viwili hivyo, Januari 16, 2017.


WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amewataka watanzania kuwapuuza watu wanaotumika na wafanyabiashara kuwapigia kampeni za biashara zao za kuuza mahindi, huku akisisitiza Tanzania ina chakula cha kutosha.
Sambamba na hilo, amekiri kupanda kwa bei kwenye baadhi ya mazao ambayo imetokana na mahitaji yaliyopo nchi za jirani ambazo zinategemea kupata chakula kutoka Tanzania.
Akizungumza na waandishi wa habari jana, mara baada ya kuzindua safari za ndege aina ya Bombardier Q400 kwa mkoa wa Dodoma, alisema taarifa zinazotolewa kuhusu hali ya chakula nchini si sahihi kwa kuwa  serikali ndio yenye jukumu la kutoa taarifa ya hali ya chakula nchini na si vinginevyo.
“Nataka kuwaondoa hofu watanzania kwamba kelele zinazopigwa na watu mbalimbali ikiwemo baadhi ya vyombo vya habari kuhusu hali ya chakula nchini taarifa hiyo sio sahihi, serikali ndio inajukumu ya kutangaza hali ya chakula iwe ni mbaya au nzuri,”alisema Majaliwa
Aliwataka watanzania kuisikiliza serikali wakati wowote inasema nini juu ya hali ya chakula kwa kuwa ina vyanzo vyake vya kutoa taarifa za uwepo wa chakula au kutokuwepo kwa chakula.
“Tunataka kuhakikishia watanzania msimu uliopita wa kilimo tulivuna chakula kingi na tulikuwa na ziada ya tani milioni 3 na ilipofikia mwezi wa 10 mwaka jana watanzania wakiwemo wabunge ni mashahidi waliomba wafanyabiashara waruhusiwe kuuza mazao yao nje ya nchi kutokana na kuwa na mazao mengi na yalikuwa hayapati soko,”alisema Waziri Mkuu
Akizungumzia kuhusu bei ya mazao kupanda, Majaliwa alikiri baadhi ya mazao kwenye masoko yamepanda bei kutokana na uhitaji wa nchi za jirani ikiwemo nchi za afrika mashariki .
“Kupanda kwa bei kunatokana na mahitaji yaliyopo nchi jirani za Kongo, Rwanda, Kenya, Somalia, Sudan hizi nchi zinategemea kupata chakula kutoka Tanzania,”alisema
Alisema hali hiyo imetokana na serikali kuzuia wafanyabiashara kupeleka mazao nje ya nchi ili Tanzania iendelee kuwa na chakula cha kutosha hadi msimu ujao.
Aidha alisema serikali inatamani kuona mkulima anauza mazao yake kwa bei nzuri na pia chakula kinapozalishwa kwa wingi pia kiuzwe kwa bei ya chini.
Hata hivyo, alibainisha serikali ilitoa kibali cha kuuzwa kwa tani milioni 1.5 nje ya nchi na tani milioni 1.5 zilizosalia ambazo zimehifadhiwa hivi sasa wameruhusu ziuzwe nchini ili kupunguza gharama ya bei sokoni.
Kuhusu hali ya mvua, alisema kwasasa mvua imeanza kunyesha kwenye mikoa yote na kuwataka wananchi kutumia mvua hizo kulima mazao ya muda mfupi na yanayostahimili ukame ili msimu ujao waweze kuvuna mazao mengi.
“Hakikisheni mnalima mazao ya muda mfupi, ili ifikapo machi au aprili waanze kuvuna na kupata chakula,”alisema Majaliwa
Hata hivyo alisema wizara ya kilimo itatoa taarifa sahihi za hali ya chakula na mazingira ya mvua kwa ajili ya msimu wa kilimo pia itatoa taarifa.
“Watanzania waondoe mashaka kuhusu hali ya chakula kwa kuwa taarifa tulizonazo kwenye mikoa juu ya hali ya chakula, chakula kipo,”alisisitiza Majaliwa
 
Copyright © 2014 Mkono Wangu Production Designed by EvMak Tanzania