Faustin Sungura
Mwenyekiti
wa Chama cha NCCR Mageuzi JAMES
MBATIA pamoja na Katibu mkuu wa chama hicho MARTINI DANDA wamepewa siku tatu kujiuzulu ndani chama hicho kwa
madai ya kujimilikisha mali za chama.
Hayo yameelezwa na aliyekuwa mmoja
wa waanzilishi na waasisi wa chama hicho baada ya madai kuwa mwenyekiti wa
chama hicho JAMES MBATIA
kujimilikisha shamba la hekhari 56 lilipo Kiromo,Bagamoyo Mkoani pwani pamoja
na nyumba 2 zilizopo Bunju B ambazo zote ni mali ya chama hicho.
Akizungumza na wahandishi wa habari
jijini Dar es salaam muanzilishi wa chama hicho FAUSTIN SUNGURA amesema mali
hizo zote walizinunua mwaka 2002 kama moja ya mali za chama kwa makubaliano
maalum.
Aidha SUNGURA amesema kuwa endapo hawatajiuzulu
ndani ya siku tatu atafungua kesi ya
jinai mahakamani kama mwendesha mashtaka wa kujitegemea chini ya sheria kifungu namba 99 cha makosa ya
jinai.
Hata hivyo amewaomba wanachama na
wapenda haki na bila kujali itikadi wamuunge mkono kwa hali na mali katika
harakati za kurudisha hadhi ya NCCR-mageuzi kwa kumuondoa mwenyekiti wa chama
hicho.
Post a Comment