CURRENT NEWS

Monday, February 27, 2017

HALI SI SHWARI SUDAN KUSINI,NJAA KALI

Ukubwa wa janga la njaa katika Jimbo la Unity nchini Sudan Kusini hali hii imebainishwa na kitenga cha umoja wa mataifa cha usambazaji misaada pamoja na familia ambao wameweza kufikiwa .
Wanawake wameweka bayana siku ambazo waliishi kwa wiki kadhaa katika mabwawa na kwamba wameyanusuru maisha yao kwa kula maua yapatikanayo kwenye mabwawa na majini, wakati mwingine matunda ya mawese na asali ya mwituni.
Mwandishi wa BBC alikuwa katika eneo la tukio katikati mwa mji wa Leer ameeleza kwamba watoto wengi wanasumbuliwa na utapiamlo.
Umoja wa mataifa kwa sasa wako kwenye mazungumzo na waasi wa Sudani Kusini kutoa mwanya wa misaada ya kwanza kufikishwa katika maeneo wanayoyadhibiti.
Inadaiwa kwamba njaa hiyo ni matokeo ya vita vya wenyewe kwa wenyewe ambayo haijawahi kutokea popote ulimwengu imepiganwa kwa miaka sita mfululizo.
Kitengo cha umoja wa mataifa kinachojishughulisha na majanga yasabishwayo na ukame na njaa kimedai kwamba kumekuwa na ongezeko kubwa la idadi ya watu walioikimbia Sudan Kusini tangu mwanzoni wa mwaka huu.
Kwa mujibu wa umoja wa mataifa takribani watu milioni tano wanahitaji msaada wa chakula haraka sana.Maelfu ya watu walikusanyika kupokea misaada iliyosambazwa kwa ndege za shirika la chakula duniani mwishoni mwa wiki.
George Fominyen ni miongoni mwa wafanyakazi , anelezea hali ilivyokua.''hapa , tulichoona ni watu wengi kufurika na wanasema walikua hawali vizuri, walikua wakitegemea maji , walikua waiketegemea mizizi na magugu maji kutoka ziwani na walikula mara moja tu kwa siku. Ni hali ngumu sana na tuna matumaini kuwa misaada ya kibinadamu itawafikia wafikia watu hawa''
Sara David anasema kuwa watu wanakufa na njaa''nyumbani hatuna chakula cha kutosha na kuna vita , tuna matatizo mengi mengi sana nyumbani, lakini sasa tunahitaji vyakula na tutamaliza matatizo yetu''
naye Nyaluat Chol Marap anasema kuwa wafanyabiashara wanajinufaisha kutokana na hali hiyo.''labda wakati fulani wafanyabiashara wanakataa kutupa chakula na bei zao wanazotutajia ni ghali mno , wanaweza kukwambia ulipe 185 hela ya sudani kwa kilo moja tu, na ukitaka kilo mbili unalipa 360 na haipatikani kwetu'
 
Copyright © 2014 Mkono Wangu Production Designed by EvMak Tanzania