CURRENT NEWS

Saturday, February 18, 2017

MAZOEZI YA VIUNGO IRINGA NI JUMAMOSI TATU ZA KILA MWEZI ,JUMAMOSI YA MWISHO NI USAFI - RC MASENZA

Mkuu  wa  mkoa  wa Iringa  Amina Masenza (  wa nne kulia)  akiwa na viongozi mbali mbali  katika mazoezi ya  viungo  leo asubuhi kutoka kulia ni mkuu wa wilaya ya  Iringa Richard  Kasesela ,kamanda wa polisi mkoa  wa Iringa Julius Mjengi   na  viongozi  wengine
Mkuu  wa  mkoa wa  Iringa Amina Masenza wa tatu  kulia  akiwa na afisa  ushirika  mkoa  wa Iringa John Kiteve na mkuu wa  wilaya ya  Kilolo Asia Abdala leo katika mazoezi  uwanja wa  Samora
Askari  na  wananchi  Iringa  wakiwa katika mazoezi
Dc  Iringa  Richard Kasesela  kulia akiwaelekeza  wananchi  mbali mbali  waliofika katika mazoezi namna ya kufanya mazoezi  kutoka  kushoto ni  mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza ,mkuu wa wilaya  Kilolo Asia Abdalah na afisa ushiriki  mkoa  John Kiteve
Kamanda  wa polisi  mkoa wa Iringa  Julius Mjengi  akishiriki mazoezi  leo
Mkuu  wa  wilaya ya  Kilolo Asia Abdalah  kulia na mkuu wa mkoa  wa Iringa Amina Masenza kushoto  wakifanya mazoezi uwanja wa Samora  na wananchi  wengine  leo
Mtumishi  ofisi ya  mkuu  wa mkoa Michael akifanya  mazoezi huku akinywa maziwa ya Asas


Afisa  takwimu  mkoa wa Iringa Hilda Kimaro wa  pili kulia  akiwajibika  na watumishi  wenzake
Mratibu wa SPANEST  Godwell  Ole Menataki mwenye jezi za Taifa  akiwajibika

Na MatukiodaimaBLOG
SERIKALI ya  mkoa  wa  Iringa  imetangaza  kuanzia  sasa mazoezi  itakuwa  mara  tatu kwa maana ya  jumamosi  tatu za  kila mwezi na jumamosi ya  nne ni  siku ya  usafi  kwa  wote  kwenye  maeneo yao .

Mkuu  wa  mkoa  wa Iringa  Amina Masenza  ametoa agizo hilo  leo  mara  baada ya  kumalizika mazoezi  ya pamoja kama  utekerlezaji wa agizo la  makamu wa  Rais la  kutenga  jumamosi  moja kwa  ajili ya mazoezi  japo mkoa  wa Iringa umekwenda  mbali zaidi kwa  kutenga  jumamosi tatu za mazoezi kwa  kila mwezi .

Alisema  kuwa  kila mtumishi wa  serikali ni lazima   kutekeleza  agizo  hilo  na kuwataka  wananchi wote wa mkoa wa Iringa  kushiriki mazoezi hayo ambayo yanafaida  kubwa kwa afya  zao hasa  kuepukana na magonjwa  yasiyoambukizwa .


Hata   hivyo  mkuu  huyo wa mkoa  amepongeza jitihada za  mkuu wa wilaya ya  kilolo Asia Abdalah ambae  ametoka  wilaya  ya  Kilolo na  kufika  kushiriki mazoezi hayo pamoja na mkuu wa  wilaya ya  Iringa Richard kasesela  ambaye  kila mara  amekuwa  akishiriki .

Pia  alishukuru  jeshi la  polisi mkoa  wa Iringa  chini ya kamanda wa  polisi  mkoa Julius Mjengi kwa  kuendelea  kuwa  chachu ya  uhamasishaji wa mazoezi  hayo .
 
Copyright © 2014 Mkono Wangu Production Designed by EvMak Tanzania