CURRENT NEWS

Monday, February 20, 2017

MEYA WA JIJI LA DAR ES SALAAM AOMBA BUSARA ZA MASHEHE NA WAZEE KATIKA KULIONGOZA JIJI HILO

Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es Salaam,Isaya Mwita,akisalimiana na Mwenyeji wake,Daluwesh Dume (katikati) kwenye hafla ya sherehe ya Maulid ya Mtume S.A.W iliyofanyika Mtaa wa Da Estate eneo la Kinondoni jijini Dar es Salaam jana. 
Meya wa Jiji la Dar es Salaam,Isaya Mwita akiwa na Diwani wa Kata ya Kinondoni,Mustapha Muro wakifuatilia kwa umakini sherehe hizo.Watoto nao hawakuwa nyuma katika shughuli hiyo.Mawaidha yakiendelea kwenye sherehe hiyo ya kuzaliwa kwa Mtume Mohamed S.A.W
Imamu Mkuu wa Msikiti wa Kinondoni Mkwajuni,Almasi Saidi,akitoa mawaidha katika sherehe hizo za kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Mtume Mohamad S.A.W katika Mtaa wa Ada Estate wilayani Kinondoni jijini Dar es Salaam leo. (PICHA ZOTE NA ELISA SHUNDA)


Imamu Mkuu wa Msikiti wa Kinondoni Mkwajuni,Almasi Saidi,Meya wa Jiji la Dar es Salaam,Isaya Mwita (katikati) na Diwani wa Kata ya Kinondoni,Mustapha Muro wakifuatilia kwa makini sherehe hizo.


 

Diwani wa Kata ya Kinondoni,Mustapha Muro,akizungumza katika maulid hiyo ya sherehe ya kuzaliwa kwa Mtume Mohamad S.A.W.Kushoto ni Meya wa Jiji la Dar es Salaam,Isaya Mwita.
Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es Salaam,Isaya Mwita,akizungumza katika hafla ya ufunguzi wa sherehe ya Maulid ya Mtume Mohamed S.A.W iliyoandaliwa na Muumini wa Dini hiyo Daluwesh Dume iliyofanyika Mtaa wa Ada Estate eneo la Kinondoni jijini Dar es Salaam leo. Katikati ni Diwani wa Kata ya Kinondoni,Mustapha Muro.Wananchiwaliohudhuria katika sherehe hizo za kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Mtume Mohamad S.A.W


Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es Salaam,Isaya Mwita,akizungumza katika hafla ya ufunguzi wa sherehe ya Maulid ya Mtume Mohamed S.A.W iliyoandaliwa na Muumini wa Dini hiyo Daluwesh Dume iliyofanyika Mtaa wa Ada Estate eneo la Kinondoni jijini Dar es Salaam leo. Katikati ni Diwani wa Kata ya Kinondoni,Mustapha Muro.


Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es Salaam,Isaya Mwita,akizungumza katika hafla ya ufunguzi wa sherehe ya Maulid ya Mtume Mohamed S.A.W iliyoandaliwa na Muumini wa Dini hiyo Daluwesh Dume iliyofanyika Mtaa wa Ada Estate eneo la Kinondoni jijini Dar es Salaam leo. Katikati ni Diwani wa Kata ya Kinondoni,Mustapha Muro na Muandaaji wa kumbukizi hiyo,Daluwesh Dume.


Kikundi cha Al Farouq kikipiga dufu wakati wa sherehe ya Maulid ya Mtume Mohamed S.A.W iliyoandaliwa na Muumini wa Dini hiyo Daluwesh Dume iliyofanyika Mtaa wa Da Estate eneo la Kinondoni jijini Dar es Salaam leo.

MEYA wa jiji la Dar es Salaam, Isaya Mwia amewaomba Mashehe na Wazee wa jiji kumuunga mkono katka shughuli anazofanya ili kuweza kutatua changamoto zilizopo katika jiji hili.

Meya Isaya ametoa kauli hiyo jiji hapa leo wakati wa maulidi ya kusherehekea kuzaliwa kwa Mtume wao Muhammad Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam ambapo pamoja na mambo mengine amesema kwama jiji la Dar es Salaam bila dua za waze, mashehe na viongozi wote wadini huwezi kuliongoza kutokana na changamoto zilizopo.

“ Najua changamoto zilizopo kenye jiji hili ni nyingi wazee wangu naomba mnisaidie sana, peke yangu siwezi, dua zenu na ushauri wenu ndio unaweza kunisaidia mimi kufanya mambo mazuri” na wananchi wakaishi kwenye mazingira wanayopenda” amesema Meya Isaya.

Leo hi mimi nikiwa na kiburi kweu kwa ajili ya madaraka haya ambayo nyie ndio mlionipa, sitaweza kutatua changamoto hata moja,zipo changamoto za kimiundombinu ya elimu, na nyingine, ambazo zote zinahitaji kupatiwa ufumbuzi, nawaombeni saa waze wangu mnipe baraka zenu” aliongeza.

Akizungumzia suala la maadili Meya Isaya amesema wazazi hawana budi kuwasaidia walimu, serikali na viongozi kwa ajili ya malezi bora hususani wakiwa shuleni.

Amesema ni jambo la ajabu na mtihani mkubwa kwa walimu ikiwa mzazi atakuwa mstari wa mbele kumnunulia mwanae simu hali yakuwa yupo masomoni jambo ambalo linafanya ashindwe kuzingatia masomo na badala yake kushinda kwenye mitanda ya kijami.

“ Leo hi mzazi unapomnunulia mwanao simu wakat unajua kabisa anasoma, huu simtihani jamani, leo hii mzazi unaposhindwa kufuatilia maendeleo ya mtoto wako shuleni huu simtihani jamani, nawaombeni sana tusaidiane kulea watoto wetu” ameongeza Meya Isaya.

Aidha Meya Isaya amewataka vijana kuacha tabia a kukaa vijiweni badala yake wajikite kwenye kufanya kaz, huku akiwaaka wazazi kutokufumbia maco vijana wao aba hatawai kujishuguisha.

Amesema vijana waliowengi hawataki kujishugulisha na badala yake husubiri kila abacho wazazi wa hutafuta jamo abalo humjengea kijana mazingira ya watto kuanza kugawaa mali kaba ya wazazi hawaja toweka duniai.

“ Wazazi msiwavumilie vijana wenu ambao wanasubiri nyie muende mkatafute wao waje wale, leo hii nyumbani unakuta baba, au Mama anapishana na kijana wake ambaye angekuwa anajitegemea mwenyewe, lakini kuendelea kuishi nao nyumbani mnataka kuwaongezea umasikini” amesema Meya Isaya.

Matokeo yake, unakuta kijana anasema Baba unakufa lini, am wanaanza kugawana mali ambazo mmetafuta nyinyi, kabla hata bado hamjatoweka duniani, jambo hili jamani sio mtihani ndugu zangu?, lazima tuwalee watoo wetu kwenye misingi ya kuwaeleza kwama dawa ya kupambana na umasikini kufanya kazi” amesisitiza.

Hata hivyo Meya Isaya amewaomba wananchi wa jiji la Dar es Salaam kutunza mazingira ili kuepukana na magonjwa ya mlipuko ikiwemo kipindupindu.
 
Copyright © 2014 Mkono Wangu Production Designed by EvMak Tanzania