CURRENT NEWS

Thursday, February 9, 2017

MNADA WA TANZANITE

Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo na baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini wametembelea Mnada wa Pili wa Kimataifa wa madini ya Tanzanite ili kujionea jinsi mnada husika unavyoendeshwa na kuwata wadau wa tanzanite kujitokeza kwa wingi katika mnada huo.
Mnada huo wa kimataifa unafanyika katika Kituo cha Jimolojia kilichopo mkoani Arusha, kuanzia tarehe 9 hadi 12, Februari, 2017 na kushirikisha wauzaji na wanunuzi mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi.
 Taarifa zaidi na...... kutoka mkoani Arusha.( pause)
Wanunuzi na wauzaji wa madini ya Tanzanite kutoka ndani na nje ya Tanzania wakiendelea na zoezi la kuangalia ubora na thamani ya madini ya Tanzanite ili kujipangia bei ya kununua madini hayo wakati wa zabuni ya kumpata mshindi wa kununua madini hayo.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo pamoja na baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini wametembelea Mnada huo  wa Pili wa Kimataifa wa madini ya Tanzanite ili kuona namna mnada huo unavyofanyika katika katika Kituo cha Jimolojia kilichopo mkoani Arusha, ambapo pamoja na mambo mengine, Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo alitoa wito kwa wadau wa madini.( Pause)
Mkurugenzi wa Kitengo cha Uthaminishaji almasi na Madini ya vito Wizara ya Nishati na Madini (TANSORT), Archard Kalugendo, amesema kuwa lengo la mnada huo ni kuhakikisha kuwa madini ya Tanzanite yanapata soko rasmi na Serikali kupata mapato yake stahiki.( pause)
 Mathius Lyatuu ni Mmoja wa washiriki katika mnada huo,( PAUSE)
Mnada wa kwanza wa madini ya Tanzanite ulifanyika mwezi Agosti mwaka 2016 ambapo jumla ya gramu 318,033.17 na karati 3,274.70 za Tanzanite ziliuzwa na jumla ya kampuni 43 kutoka mataifa mbalimbali duniani zilihudhuria.
Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge  waliotembelea mnada huo ni pamoja na John Heche Mbunge wa Tarime Vijijini, Catherine Magige Mbunge wa viti maalum,CCM, mkoani  Arusha, Mwantakaje Juma Mbunge wa Bububu na Dunstan  Kitandula Mbunge wa Mkinga.
 
Copyright © 2014 Mkono Wangu Production Designed by EvMak Tanzania