CURRENT NEWS

Saturday, February 11, 2017

RC IRINGA AINGIA DARASANI KUFUNDISHA , AAGIZA WILAYA YA MUFINDI KUINGIA 10 BORA UFAULU KITAIFA

Mkuu  wa  mkoa wa Iringa mwalimu  Amina Masenza akifundi somo  la Uraia kwa  wanafunzi wa  kidato  cha tano  shule ya  sekondari  Sadani  wilaya ya  Mufindi leo baada ya  kufanya  ziara  shuleni hapo
Mkuu wa mkoa wa Iringa Mwalimu Amina Masenza  akifundisha somo la urai
Mkuu  wa mkoa wa  Iringa mwalimu Amina Masenza akipokelewa  shule ya sekondari Sadani
Mkuu  wa  wilaya ya   Mufindi Wiliam Jamhuri akimkaribisha  mkuu wa mkoa wa Iringa
Watalam  wa  mkoa wa Iringa
Walimu na viongozi wa wilaya ya  Mufindi
Watumishi  wakimsikiliza  mkuu wa mkoa
Mkuu  wa  shule ya  sekondari  Sadani Mufindi Yusuph Mwagala
Mkuu  wa  shule ya  sekondari  Sadani Mufindi Yusuph Mwagala akipongezwa na mkuu wa  mkoa  wa Iringa Mwalimu Amina Masenza 
Mkuu wa mkoa  wa Iringa mwalimu Amina Masenza na mkuu wa  wilaya ya  Mufindi Wiliam Jamhuri  wakifungua daharia  ya  wasichana  shule ya  sekondari Sadani
Rc  akikagua  daharia  hiyo
Bwalo la chakula  Sadani  Sekondari  ambalo linahitaji wadau  kuchangia ili kukamilika
Rc Mwalimu Masenza  akitoka kukagua  bwalo  hilo
Mwanafunzi wa kidato cha  sitta  Sadani  sekondari Sagendo Fadhili  akijibu maswali ya  mkuu wa mkoa wa Iringa Mwalimu  Amina Masenza
Mkuu  wa mkoa wa Iringa  Mwalimu Amina Masenza  akiendelea  kufundisha  wanafunzi wa  kidato cha nne   shule ya  sekondari  sadani
Mkuu  wa mkoa wa Iringa mwalimu Amina Masenza akiwa na mkuu wa shule ya Sadani katikati na mkuu wa wilaya ya Mufindi Bw Wiliam Jamhuri  kushoto
Walimu  wa  Sadani Sekondari  wakifurahia  ziara ya mkuu wa mkoa shuleni hapo na kuomba kusaidiwa  kusogezewa  umeme wa  Rea  shuleni hapo
Mwalimu Masenza mkuu wa mkoa  wa Iringa  akiteta na  walimu wenzake wa  shule ya  sekondari Sadani Mufindi
Mkuu  wa mkoa  wa Iringa Mwalimu Amina Masenza (wa nne kushoto)  akiwa katika  picha ya pamoja na walimu wa  shule ya  sekondari  Sadani

Na  MatukiodaimaBlog

MKUU  wa  mkoa wa  Iringa Amina Masenza amelazimika  kuingia darasani kufundisha kama njia ya kuwataka walimu kuwajibika kufundisha  huku akiuagiza uongozi wa  wilaya  ya Mufindi kuhakikisha wanaweka mikakati itakayoiwezesha  shule ya sekondari ya Sadani kuingia katika nafasi  ya 10 bora katika mitihani ya kitaifa mwakani  2018.
Huku akichangia  kiasi  cha Tsh milioni 1 kwa ajili ya ujenzi wa bweni la  wanafunzi  shuleni hapo  kama sehemu ya maandalizi ya shule   hiyo kujiandaa kuwa shulebora kitaifa.

Mkuu  huyo  wa mkoa ametoa agizo hilo  leo wakati wa ziara  yake ya  ukaguzi na ufunguzi wa  bweni la wanafunzi wa  kike  katika  shule  hiyo,kuwa kutokana na mkoa  wa  Iringa  kufanya vema  katika  mitihani ya Kitaifa ya  kidato  cha  nne kwa  kuwa mkoa wa pili kitaifa ila bado wilaya ya Mufindi  inapaswa kuhakikisha shule  hiyo  kuwa  kati ya shule  10 bora kitaifa .
Alisema  kuwa  moja katika ya maagizo ambayo anataka mkurugenzi  wa Halmashauri ya  wilaya ya Mufindi kufanya ni kuandaa mkataba  maalum, kati ya  waslimu  wa shule  hiyo ya mkurugenzi mkataba ambao atausaini kwa  ajili ya ofisi yake na mkuu wa wilaya ya Mufindi kuingia mkataba iwapo watashindwa  kuingia katika  shule 10 bora basi watamtafuta aliyekwamisha mkataba illi achukuliwe hatua.

“ Mkataba  hii itakuwa kwa  walimu wote  wa mkoa wa Iringa ili kupima uwezo wa  walimu katika kutimiza wajibu  waokatika utendaji kazi  ili kama mwalimu asiyewajibika basi  kukaa pembeni ili kupisha mwalimu ambae anafanya kazi  kwa ari ya  kujituma zaidi”


Hata hivyo aliwataka  walimu kufanya kazi  kwa  kutimiza  wajibu wao     badala ya  kufanya kazi  kwa  mazoea kwa  kukimbilia  kudai haki  zao badala  ya kufuata  taratibu.

Alisema  wapo  baadhi ya  walimu  wanalalamika kudai haki  zao  ila wamekuwa wakiendea  kutibiwa nje ya  mkoa  bila  hata ya  kufuata taratibu za kuandika barua na  kuwataka  kuzingatia  taratibu  za  kazi kwa kutunza  kumbukumbu  mbali mbali katika mafaili  yao.

Kuhusu ujenzi  bweni na umaliziaji  wa bwalo la chakula  shuleni hapo  aliagiza  mkuu  wa  wilaya  kuitisha kikao  na wafanyabiashara   ili  kusaidia ujenzi huo na shughuli za  kimaendeleo shuleni hapo.

Pia  alipongeza jitihada  kubwa  zinazofanywa na uongozi  wa  shule  hiyo  chini  ya mkuu wake Yusuph Mwagala kutokana  na kuendelea  kufanya shule  hiyo  kuwa mbeli  kielimu pamoja na  maendeleo mengine
Awali mkuu  wa  shule  hiyo Bw Mwagala  alisema  kuwa  shule  hiyo  imeendelea  kufanya  vema  katika nafasi ya  kimkoa na  kitaifa  ambapo   mwaka  2015 katika  matokeo  ya kidato  cha nne ilishika  nafasi  ya 64 kati ya shule 131 kimkoa na kiwilaya ilishika nafasi ya 26 kati ya shule  54 wakati kwa mwaka  huu imeshika nafasiya 25 kati ya  shule 152 kimkoa na nafasi ya 8 kati ya 42 kiwilaya

Pia  alisema  mbali ya mafanikio katika  elimu  bado  shule  hiyo inakabilia na changamoto mbali mbali kamaupungufu  wa mabweni  ya  wanafunzi wa kidato cha tano na  sita upungufu ambao  unatokana na  ongezeko  kubwa  la  udahiri  wa  wanafunzi wa  kidato cha tano kulingana  na  miundo mbinu iliyopo kabla ya  kuanzisha kidato  cha tano na  sita ,upungufu  na uchakavu wa vyumba  vya  madarasa,ukosefu  wa  umeme ,ukosefu  wa bwalo  la  chakula, upungufu wa  walimu  8 wa masomo ya sayansi  ,walimu watatu  wa somo la biolojia, walimu   wawili  wa masomo ya fizikia ,walimu  watatu  wa kemia  na  hesabu  mwalimu mmoja ,ukosefu wa  maabara ya  biolojia.

MWISHO
 
Copyright © 2014 Mkono Wangu Production Designed by EvMak Tanzania