CURRENT NEWS

Friday, February 24, 2017

RPC PWANI -TUTAKESHA KUWASAKA WALIOFANYA MAUAJI KIBITI

KAMANDA wa polisi mkoani Pwani, Boniventure  Mushongi, akizungumzia tukio la  mauaji lililotokea wilayani Kibiti mkoani Pwani (Picha na Mwamvua Mwinyi)

Na Mwamvua Mwinyi, Kibiti
KAMANDA wa jeshi la polisi mkoani Pwani, Boniventure Mushongi, amesema jeshi hilo kwa kushirikiana na makachero wake linaendelea na msako mkali kuwasaka waliohusika katika tukio la mauaji lililotokea feb 21 huko Jaribu Mpakani, kata ya Majawa, Kibiti.
Aidha ameeleza kwamba, taarifa zaidi juu ya matokeo ya msako huo zitatolewa wakati wowote mara baada ya kuwabaini wahalifu hao.
Katika tukio hilo, watu watatu walipoteza maisha ambapo mmoja kati yao akiwa OC CID Kibiti baada ya kuuwawa na  kundi la watu wanaodhaniwa ni majambazi wakiwa na silaha aina ya SMG/SAR .
Kamanda Mushongi alisema tukio hilo limetokea feb 21 majira ya saa  mbili usiku  ambapo  watu sita  walivamia katika kituo cha ukaguzi wa mazao ya misitu na kuwauwa watu watatu .
Waliouawa ni pamoja na OC CID wilaya ya Kibiti sp.Peter Kubezya ambae alipigwa risasi kwenye kiuno .
Alitaja wengine kuwa ni Peter Kitundu Mkaguzi wa maliasili kituo cha Jaribu  Mpakani na mgambo  aliyekuwa akifanyakazi za ulinzi kwenye kizuizi hicho, Athumani Ngambo .
Kamanda Mushongi alisema wote hao wawili waliuawa kwa kupigwa  risasi kichwani na begani na kupoteza maisha papo hapo .
"Upelelezi na operesheni zinaendelea usiku na mchana ili kuhakikisha waliofanya tukio hilo wanapatikana "alisema.
Alifafanua ,katika eneo la  tukio kulikutwa pikipiki mbili namba  MC 853 AHH aina ya Toyo na MC 799 aina ya Sunlg na kipeperushi chenye ujumbe wa kitisho .
Mwisho
 
Copyright © 2014 Mkono Wangu Production Designed by EvMak Tanzania