CURRENT NEWS

Friday, February 10, 2017

SHARIF-SIASA ZA KUBEZANA ZIMEPITWA NA WAKATI KILICHOPO NI KUPIGA KAZI


 Halid Chokoraa akitumbiza katika kampeni za uchaguzi mdogo wa kitongoji cha Magomeni B, kata ya Nianjema, Bagamoyo, wakati wa kumnadi mgombea kupitia CCM Rajab Swedy (picha na Mwamvua Mwinyi)
Meneja wa kampeni za uchaguzi mdogo kitongoji  cha Magomeni B ,kata ya Nianjema ambae pia ni Mwenyekiti wa jumuiya ya wazazi Bagamoyo, Alhaj Abdul Sharif akimnadi mgombea kupitia CCM Rajab Swedy. ( picha na Mwamvua Mwinyi)

Na Mwamvua Mwinyi,Bagamoyo
MENEJA wa kampeni katika uchaguzi mdogo wa kitongiji cha Magomeni B,kata ya Nianjema wilayani Bagamoyo,alhaj Abdul Sharif amesema maendeleo ya nchi hayaitaji siasa za kubezana wala kutusi chama kingine.
Amesema ni wakati wa vyama vya upinzani kubadilika na kuachana na tabia ya kuzusha hoja ama kubeza chama kilichopo madarakani na badala yake vijipange kutumikia wananchi kwa sera na vitendo.
Alhaj Sharif ,ambae pia ni mwenyekiti wa jumuiya ya wazazi Bagamoyo,aliyasema hayo katika muendelezo wa kampeni za kitongoji hicho.
Alisema ,wakati  kampeni hizo zikiendelea wilayani hapo,baadhi ya vyama vya upinzani ikiwemo CUF kimekuwa kikikitusi chama cha mapinduzi majukwaani na kudai hakuna ilichofanya ndani ya miaka 40.
Alhaj Sharif alielezea kuwa,inaonyesha dhahiri kuwa chama hicho kinavyofilisika kisiasa ,.Kwani kinapaswa kushindana kwa hoja na sera na sio kutukana jambo ambalo halina tija kwa jamii.
“Rajab Swedy,tumemsimamisha kupitia  chama cha mapinduzi,hatuna shaka nae, ana uwezo kiuongozi,hana skendo yeyote na ana sifa ya kuongoza kitongoji hiki”
“Naomba mmpe kura za ndio siku ya uchaguzi februari 19,kwani chama alichopitia kinafanya mengi nchini,kinatatua kero mbalimbali ,kinabana wabadhilifu na wakwepa kodi kila kona ili kurejesha fedha za wananchi”alisema .
Alifafanua ,hakuna asiyeona mambo yanayofanywa na CCM kuanzia ngazi za chini na Taifa na namna rais John Magufuli anavyopigania maendeleo na wanyonge.
Nae diwani wa kata ya Yombo,Mohammed Usinga ,alisema ni wakati wa vyama pinzani kuzikwa kabla ya kufikia uchaguzi mkuu 2020 .
Usinga ambae pia ni makamu mwenyekiti wa halmashauri ya Bagamoyo, alieleza kwamba,vyama hivyo vimekuwa kama ndege kulimbizi,.Ambapo wanakibeza chama ambacho wanatumia ilani yake ,barabara,madawa,maji yanayoletwa na CCM.
Hata hivyo alisema endapo atachaguliwa Swedy halmashauri itafanya nae kazi kwa ukaribu zaidi kutokana na madiwani wote kutoka CCM.
Usinga aliwaomba wananchi wamchague mgombea huyo ili kuwarahisishia viongozi hao waweze kuwatumikia kwa kutekeleza ilani moja bila kuchanganya madawa.
Kwa upande wake mgombea nafasi ya mwenyekiti kitongoji cha Magomeni B,Swedy alisema amelelewa kwenye makuzi ya chama ambacho kina maadili hivyo hawezi kufanya kampeni za kutukana mtu.
Alisema amekuwa akitukanwa na kuzushiwa mengi yasiyokuwepo ili kuchafuliwa lakini amewaomba wananchi wa kitongoji hicho kuyapuuza na kumchagua februari 19 mwaka huu.
Swedy aliahidi kuitendea haki ilani ya chama cha mapinduzi kwa kushirikiana na viongozi wenzie wa chama ,serikali na halmashauri ili kuleta maendeleo chanya ndani ya kitongoji hicho
 
Copyright © 2014 Mkono Wangu Production Designed by EvMak Tanzania