CURRENT NEWS

Saturday, February 18, 2017

WANANCHI NA WANACCM WATAKIWA KUJITOKEZA KWA WINGI KWENYE UCHAGUZI WA VITONGOJI FEB 19

Meneja wa kampeni za uchaguzi mdogo kitongoji  cha Magomeni B(CCM) ,ambae pia ni Mwenyekiti wa jumuiya ya wazazi Bagamoyo, Alhaj Abdul Sharif akifunga kampeni hizo kwa kumnadi mgombea kupitia CCM Rajab Swedy. ( picha na Mwamvua Mwinyi)


Na Mwamvua Mwinyi, Bagamoyo
WANACHAMA wa chama cha mapinduzi (CCM) na wananchi kijumla ,wametakiwa kujitokeza kwa wingi katika uchaguzi mdogo wa vitongoji unaotarajiwa kufanyika februari 19 ikiwemo kitongoji cha Magomeni B, kata ya Nianjema Bagamoyo.
Aidha vijana wametakiwa kuacha kugeuzwa kuwa walinzi wa kura zilizopigwa badala yake waachie kazi hiyo ifanywe na vyombo dola.
Akifunga kampeni za CCM kitongoji hicho, jana meneja wa kampeni hizo, alhaj Abdul Sharif, kampeni zimemalizika wananchi wafanye maamuzi yasiyo na majuto.
"Rajabu Swedy anajiuza na sera za chama tawala zinazotekelezeka, sera makini hivyo haina budi kumchagua kwa kura nyingi "
"Wapinzani wameishiwa na sera wamebakia kutusi majukwaani ikiwa ndio agenda yao kuu ambayo haina mashiko"alisema alhaj Sharif.
Alhaj Sharif alieleza kwamba CCM imejipanga kutatua kero za wananchi ili kuleta maendeleo.
Aliwaasa wanachama wa vyama vya upinzani kuacha tabia ya kubeza masuala yanayotekelezwa na serikali iliyopo madarakani chini ya rais dk. John Magufuli.
Alhaj Sharif alisema mwenye macho aambiwi tazama kwani kila mmoja anaona jinsi rais na watendaji wake wanavyochapa kazi na kudhibiti mianya ya rushwa, ubadhilifu na ukwepaji Kodi kwa maslahi ya jamii.
Nae mgombea nafasi ya mwenyekiti kitongoji cha Magomeni B Rajabu Swedy aliomba wananchi wa kitongoji hicho wamuamini.
Alisema ni wakati wa kufanya maendeleo kwa vitendo na sio bla bla zisizo na tija.
Swedy alifafanua anaahidi kutekeleza na kusimamia changamoto zinazowakabili wananchi hao kwa kushirikiana na serikali, wanaanchi, halmashauri na wadau.
Aliomba wasifanye makosa kuchagua wagombea kutoka vyama pinzani na badala yake wamchague yeye kwkuwa anauwezo wa kuongoza na chama chake kinawatumikia watanzania.
Mwisho
 
Copyright © 2014 Mkono Wangu Production Designed by EvMak Tanzania