CURRENT NEWS

Saturday, March 11, 2017

DC MTATURU ATOA WIKI MOJA KWA MKURUGENZI WA HALMASHAURI KUWASILISHA TAARIFA YA UJENZI WA MAABARA YA SEKONDARI YA MUNKINYA.


Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Miraji Mtaturu akiwa kwenye picha ya pamoja na Padre Francis Limu (kulia) Das Ikungi Winfrida Funto na (kushoto) kwake ni  Diwani wa kata ya Dung'unyi Richard Nkhangaa,Mkiti wa Kijiji cha  Dung'unyi, kamati ya ulinzi na salama na walimu wa Seminary wakati mkuu huyo alipofanya ziara shuleni hapo.
Mkuu wa wilaya ya Ikungi Miraji Mtaturu akipata maelezo toka kwa Padre Fransic Limu alipotembelea darasa huku diwani inspector Ponsiano na katibu tawala wa wilaya hiyo Winfrida Funto wakisikiliza.

Jumuiya wanafunzi wa Seminary ya Dung'unyi wakimsikiliza kwa makini mkuu wa wilaya ya Ikungi hayupo pichani mara baada ya kupata nafasi  ya kuongea nao alipopita kwenye shule  hiyo.
Mkuu wa Seminari ya Dung'unyi  Padri Fransic  Limu akitoa ufafanuzi kwa mkuu wa wilaya ya Ikungi Miraji Mtaturu alipokuwa kwenye ziara yake shuleni humo.

\Padre Francis Limu akimuonyesha mkuu wa wilaya ya Ikungi Miraji Mtaturu mradi wa ufugaji wa samaki uliopo katika shule ya seminari  ya Dung'unyi wakazi mkuu huyo alipokuwa kwenye ziara yake ya kila alhamisi ya kutembelea tarafa zilizopo wilayani humo.


Wananchi wa Kata ya Dung'unyi wakimsikiliza mkuu wa wilaya ya Ikungi ambaye hayupo pichani wakati alipozungumza nao kwenye mkutano wa hadhara mara baada ya kupokea kero zao. 
 Mkuu wa wilaya ya Ikungi Miraji Mtaturu akizungumza na wananchi wa kata ya Dung'unyi alipofanya mkutano wa hadhara wakati akiwa kwenye ziara.
...............................................................................
KATIKA kuhakikisha kila shule ya Sekondari inakuwa na maabara,Mkuu wa wilaya ya Ikungi Miraji Mtaturu amemtaka mkurugenzi wa halmashauri hiyo Rustika Turuka kuwasilisha taarifa kwake ndani ya wiki moja ya namna walivyojipanga kukamilisha maabara iliyopo katika shule ya Sekondari Munkinya iliyopo kata ya Dung'unyi wilayani humo.

Mtaturu alitoa agizo hilo akiwa kwenye muendelezo wa ziara zake za kila alhamisi  katika Tarafa zilizopo wilayani humo ambapo hapa alitembelea tarafa ya Ikungi kukagua miradi na kusikiliza kerpo za wananchi na kuzipatia majibu. 

“Mh. Mkuu wa wilaya hapa tuna maabara yetu ya sekondari ya Munkinya ambayo ipo kwenye hatua ya umaliziaji na kuweka vifaa vya maabara ili iweze kuanza lini maabara hii itakamilika?”,aliuliza mmoja wa wananchi Ambrose Joseph.

Akijibu maswali yao Mtaturu pia aliwahimiza wananchi hao kuendelea kushiriki shughuli za maendeleo ili kuunga mkono juhudi zinazofanywa na serikali.

Aliiomba serikali kuisaidia wilaya hiyo kuondoa ndege aina ya Kweleakwelea ambao wanaharibu mazao  ambapo kwa sasa wameanza kula Mtama shambani hali ambayo inaweza kusababisha kukosekana kwa mavuno mazuri ilhali kwa sasa mvua inanyesha vizuri na mazao ni mazuri.

Aliwataka wananchi kutumia vizuri mvua zinazoendelea kunyesha kwa kupanda mazao yanayotumia maji kwa ufanisi kama muhogo na viazi.
Katika ziara hiyo alitembelea pia shule ya seminari ya Dung`unyi iliyopo yenye sekondari kongwe ya binafsi inayomilikiwa na kanisa Katoliki na kukutana na mkuu wa Seminari hiyo padri Francis Limu ambaye katika maelezo yake alisema shule hiyo ilianzishwa mwaka 1996 ikiwa ni ya kidato cha kwanza hadi cha sita kwa michepuo ya sanaa,biashara na sayansi na inapokea pia wanafunzi kutoka ndani na  nje ya mkoa wa Singida.

Alisema kiwango cha ufaulu ni kizuri katika mitihani ya Taifa na kuiomba serikali kurekebisha barabara ya Ikungi-Dung`unyi hadi Makiungu ili barabara hiyo iweze kupitika wakati wote.

 “Mh. Mkuu wa wilaya shule yetu inapata ushirikiano mkubwa kutoka serikalini pale tunapouhitaji na tunakushukuru wewe kwa kututembelea kwa kuwa katika kipindi cha miaka mitano wewe umekuwa mkuu wa wilaya wa kwanza kututembelea,”alisema Padri Limu.

Akizungumza mara baada ya kupokea taarifa hiyo mkuu wa wilaya hiyo, alilipongeza kanisa kwa kazi nzuri ya kuwaandaa vijana kuwa raia wema,kuwaandaa kitaaluma ili kukabiliana na mazingira ya maisha yao ya baadae na kuahidi kama serikali kuendelea kutoa ushirikiano zaidi katika kuboresha taaluma wilayani humo.

“Naona hapa mna ujenzi wa kuongeza mabweni mawili ya A level na jiko sasa naomba niongezee nguvu katika hili nawachangia mifuko 30 ya saruji ili isaidie kukamilisha  ujenzi mlionao na watoto wetu wapate kusoma katika mazingira mazuri,”alisema Mtaturu.


Aliwaasa wanafunzi kuzingatia masomo na kudumisha nidhamu kwani ndio msingi wa mafanikio yao.
 
Copyright © 2014 Mkono Wangu Production Designed by EvMak Tanzania