CURRENT NEWS

Sunday, March 19, 2017

FREDRICK MWAKALEBELA ACHUKUA FOMU YA KUGOMBEA UBUNGE WA EAC

Fredrick Mwakalabela wa kulia akikabidhiwa fomu na Afisa Oganaizesheni Jackson Shalua katika ofisi za CCM Makao Makuu Dodoma hii leo 

ALIYEKUWA Mkuu wa Wilaya ya Wanging'ombe Fredrick Mwakalebela amechukua fomu ya kugombea ubunge katika Bunge la Afrika Mashariki katika Chama Cha Mapinduzi (CCM).


mwakalebela alichukua fomu leo Makao Makuu ya CCM mjini Dodoma na kueleza kuwa  kuwa sasa umefika wakati wa kuwatumikia watanzania kupitia bunge hilo kwanitakuwa teyari kuwatumika watanzania kwani anazijua changamoto za EAC."umefika wakati wa kuwatumikia watanzania kupitia bunge hili ,uwezo wa kuwatumikia ninao na changamoto mbalimbali za EAC nazijua"alisema Mwakalebela na kuongeza kuwa"Nawaomba wabunge kunipa ridhaa,kikubwa ni fursa zilizopo Afrika Mashariki na jinsi gani Tanzania itafaidika,naamini CCM inanifahamu Nina imani wataniangalia ili niweze kuwatumikia"Aidha alimpongeza Mwenyekiti wa CCM Dk John Magufuli kwa kauli yake ya kutaka wapatikane viongozi waadilifu wasiotumia rushwa na kwamba anaamini uchaguzi huo utakuwa huru na haki.Mwakalebela ambaye pia ni Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa Taifa wa CCM alisema "Uadilifu wangu unajulikana kwani nimefanya kazi sehemu nyingi  nina uzoefu wa kutosha nikifanikiwa kupata nafasi hii sitawaangusha walionichagua na watanzania kwa ujumla "Mwisho.
 
Copyright © 2014 Mkono Wangu Production Designed by EvMak Tanzania