CURRENT NEWS

Wednesday, March 22, 2017

HALMASHAURII MAMA YA RUFIJI NA YA KIBITI ZATAKIWA KUMALIZA MIGONGANO -RC NDIKILOMkuu wa mkoa wa Pwani, mhandisi Evarist Ndikilo, wa pili kutoka kushoto, akizungumza na watumishi wa halmashauri ya Kibiti kwenye muendelezo wa ziara yake mkoani humo ,wa kwanza kushoto mkuu wa wilaya ya Kibiti ,Hussein Gulam Kifu na wa kwanza kulia ni Mkurugenzi wa halmashauri hiyo, Alvera Ndebagye. (picha zote na Mwamvua Mwinyi) 

MKUU wa mkoa wa Pwani mhandisi Evarist Ndikilo, ameiagiza ofisi ya Katibu tawala Mkoani hapo (RAS), amalize tatizo la mgawanyo wa fedha na mali zilizobakia baina ya halmashauri ya Kibiti na halmashauri mama ya Rufiji.
Amesema ifikapo March 28 mwaka huu mgongano huo uwe umemalizika ili kila uande ufe na chake.
Ameeleza ni tangu mwanzoni mwa mwaka jana zilipogawanywa wilaya hizo ni kipindi kirefu hivyo kila halmashauri ipewe nafasi na uwezo wa kujitegemea.
Aidha mhandisi Ndikilo amewataka watendaji wa halmashari ya Kibiti kusimamia makusanyo kikamilifu ili kuinua mapato yao.
Maagizo hayo aliyatoa,wakati akizungumza na watumishi wa wilaya hiyo kwenye mwendelezo wa ziara yake mkoani hapo.
Alisema waziri mkuu alipita wilayani humo na kuzungumza suala hilo pamoja na kikao cha ushauri cha mkoa RCC kutoa maagizo.
Mhandisi Ndikilo, alisema licha ya wilaya hiyo kuwa mpya na kuwepo changamoto nyingi lakini ni lazima itumikie wananchi.
"Tulioigawa Rufiji na kuwa na Kibiti tulilenga kufikisha maendeleo kirahisi na sio vinginevyo "
"Hivyo watumishi na watendaji wote kila mmoja achape kazi, muache kufanya kazi kwa mazoea, watimize wajibu wao "alieleza.
Mkuu huyo wa mkoa, aliwataka viongozi wa halmashauri ,wataalamu, madiwani na wilaya ya Kibiti kushirikiana kwani hategemei migongano.
Alielezea hategemei kufikia kwenye kukinzana baina ya pande hizo.
Nae mkuu wa wilaya ya Kibiti,GulamHussein Kifu alisema tatizo linaonekana lipo kimaslahi ama utekelezaji kutoka mkoani.
Alisema haoni tatizo hadi leo kushindwa kupewa mafungu yao.
Kifu alisema wamechoshwa na kupiga magoti kwa halmashauri ya Rufiji kwa kila wanachotaka kutekeleza hivyo kusababisha kushindwa kupiga hatua kiuchumi.
Kwa upande wake, mkurugenzi wa halmashauri ya Kibiti,Alvera Ndebagye alifafanua kwamba, kunatakiwa wapate fedha za mgawanyo wa bakaa.
Alibainisha pia hawajakabidhiwa mikataba ya miradi mbalimbali kujua mchakato, na ilipofikia.
Alvera alisema hadi sasa makusanyo yanasuasua kutokana na kutokuwa kamili kufuatia mapungufu hayo.
Katibu tawala, uchumi na uzalishaji, Shangwe Twamala alisema amepokea malalamiko yaliyotolewa na maagizo ya RC.
Twamala alisema kuwa, atayafikisha ofisi husika kwenda kufanyiwa kazi.
 
Copyright © 2014 Mkono Wangu Production Designed by EvMak Tanzania