CURRENT NEWS

Saturday, March 25, 2017

KATI YA WATU 3447 WALIOJITOKEZA KUPIMA AFYA ZAO 27 WAHISIWA KUWA NA KIFUA KIKUU MUFINDI

Mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza akipata maelezo ya kasi ya upimaji VVU leo Mufindi kwenye kilele cha siku ya kifua kikuu na UKIMWI
mkuu wa mkoa akiwa banda la benki ya wananchi wa Mufindi 


Mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza akimkabidhi baiskeli zilizotolewa na Africare mtoa huduma majumbani Shukuru Ngelime leo 
 Na MatukiodaimaBlog

WAKATI Leo ni maadhimisho ya siku ya kifua kikuu Dunia imeelezwa kuwa kati ya watu 3447 waliojitokeza kupima  afya zao wilaya Mufimdi mkoani Iringa idadi ya watu 27 wahisiwa kuwa na maambukizi ya kifua kikuu.

Akitoa taarifa ya upimaji wa VVU na kifua kikuu leo wakati wa kilele cha maadhimisho hayo yaliyofanyika kimkoa  kwenye viwanja vya mashujaa mjini Mafinga wilayani Mufindi  mratibu wa Kifua kikuu na Ukimwi Mkoa Tecla Orio,alisema idadi hiyo imetokana na wale waliojitokeza kupima kwa hiari afya zao. 

Alisema kuwa kwa wakati wote ndani ya wiki Moja sasa wamekuwa wakizunguka kata mbali mbali kupima kifua kikuu na Ukimwi.

"Tulifanya kampeni ya huduma shirikishi ya ushauri nasaha na upimaji wa VVU, uchunguzi wa wagonjwa wa shinikizo la damu pamoja na huduma ya uzazi wa mpango"

Kuwa jumla ya wanawake 2019 na wanaume 1368 ndio waliopima Ukimwi na kifua kikuu na waliokutwa na maambukizi ya Ukimwi ni 49 wanawake ni 31 na wanaume 18 wakati waliohisiwa kuwa na kifua kikuu ni wanaume 12 na wanawake 15.

mratibu huyo aliena kwa upande wa shinikizo la damu kati ya watu hao waliopima kupitia kampeni hiyo ambao ni 655 walioonekana na shinikizo la damu ni watu 191 wakiwemo wanaume 85 na wanawake 106.

Kuhusu huduma ya uzazi wa mpango waliochunguzwa 139 na wanawake 139 walipatiwa huduma ya kansa ya mlango wa uzazi. 

Akiwahutubia wananchi hao mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza aliagiza wakurugenzi na wakuu wa wilaya zote mkoani Iringa kuanzisha utaratibu wa kuanzisha mikusanyiko ya utoaji wa elimu juu ya afya. 

Kuwa wapo baadhi ya watu ambao wanauelewa ndogo juu ya kifua kikuu hivyo kupitia mikusanyiko hiyo wataweza kupatiwa elimu sahihi na wanapodungulika basi kuanzishiwa tiba. 

Alisema katika mkoa wa Iringa taarifa zilizopo ni zaidi ya wagonjwa 1000 ambao hughundulika kila mwaka kati yao asilimia 40 wanayo maambukizi ya VVU. 

Hivyo aliwataka wananchi wakihisi kuwa na dalili za kifua kikuu kukimbilia hospitali ili kuanzishiwa matibabu na moja kati ya dalili za kifua kikuu mwili kupatwa joto Kali hata wakati wa baridi kali. 

mkuu huyo wa mkoa alitaja makundi ambayo yapo hatarini kupatwa na Kifua kikuu kuwa ni watu wanaoishi na VVU, watu walio katika msongamano, wazee zaidi ya miaka 65,watoto chini ya miaka mitano, watu wenye magonjwa ya muda mrefu kama kisukari, saratani na mengine 

Pia watu wenye lishe duni na walevi wa kupindukia hivyo kuwataka wananchi kupima afya zao 

Wakati huo huo mkuu wa mkoa amekabidhi jumla ya baiskeli 125 zenye thamani ya shilingi milioni 18.7 kwa watoa huduma wa afya majumbani. 

Mratibu wa shirika la Africare G.  Fund Aloyce Mkangaa alisema baiskeli hizo zimetolewa kwa wahudumu wa wilaya ya Mufindi na Iringa.
 
Copyright © 2014 Mkono Wangu Production Designed by EvMak Tanzania