CURRENT NEWS

Monday, March 6, 2017

KOKA-AWATAKA VIJANA KUJITUMA NA KUJIUNGA VIKUNDI ILI KUJIINUA KIMAENDELEO Mbunge wa jimbo la Mji wa Kibaha ,Silvestry Koka,akizindua mradi wa kuosha magari wa chama cha madereva pikipiki Mailmoja Kibaha.(Picha zote na Mwamvua Mwiny)


Na Mwamvua Mwinyi,Kibaha
MBUNGE wa jimbo la Mji wa Kibaha,mkoani Pwani,Silvestry Koka,awataka vijana kuacha kujibweteka na kuwa tegemezi,badala yake wajikite katika shughuli ndogondogo ili kujiinua kiuchumi.
Amesema anatambua tatizo kubwa ni kukosa mitaji kwa vijana lakini,nguzo pekee ya kupata msaada kirahisi ni kuunda vikundi ili kuweza kuwawezesha mikopo na masuala mengine ya maendeleo.
Koka aliyasema hayo,mjini Kibaha baada ya kuzindua mradi wa chama cha madereva wa pikipiki ,Mailmoja wa mashine ya kuoshea magari(car wash).
Aliwaomba wale walioanza ujasiliamali kuacha ubinafsi bali wawasaidie wengine wasiojua ili hali waweze kutoka kimaisha pasipo kukaa vijiweni bila kuwa na mwelekeo wowote.
Aidha Koka aliwasihi madereva hao kujenga umoja na mshikamano utakaowasaidia kulinda maslahi na faida wanazozipata.
Hata hivyo, aliahidi kuendelea kushirikiana katika kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili vijana na makundi mengine ikiwemo wanawake ili kuweza kupiga hatua kiuchumi jimboni humo.

Mbunge huyo,alifafanua kwamba tangu aanze uongozi wake ameshasaidia makundi mbalimbali ya ujasiliamali ya wanawake na vijana zaidi ya sh.mil.180 kutoka mfukoni mwake.
“Nimejipanga kuendelea kuviwezesha vikundi hivyo kwani ni moja ya kutimiza vipaombele vyangu nilivyojiwekea japo kuwa vijana bado hawajajipanga kikamilifu”alieleza Koka.

Awali,Koka alizungumza na wajumbe wa kamati ya siasa kata ya Mailmoja na anaendelea na ziara yake aliyoianza jimboni hapo.
 
Copyright © 2014 Mkono Wangu Production Designed by EvMak Tanzania