
Na Woinde
Shizza,Arusha
Wanawake wote hapa nchini wametakiwa kujijengea tabia ya
kupima afya zao mara kwa mara ili kuweza kujua matatizo ya mwili waliyonayo na kuyatatua kabla ya madhara makubwa kutokea .
Hayo yamebainishwa leo na
mkurugenzi wa kampuni ya
Phide entertaiment Phidesia Mwakitalima wakati alipokuwa
akiongea na waandishi wa habari juu ya maandalizi ya wiki wanawake duniani ambayo inatarajia kuanza
March mbili ambapo kwa mkoa wa Arusha maadhimisho hayo yanatarajiwa kufanyika
kwa muda wa siku saba katika viwanja vya
kumbukumbu ya sheikh Amri Abeid .
Alisema kuwa wanawake wengi wamekuwa awana tabia ya
kupima afya zao mara kwa mara kitu
ambacho ni hatari mno kwani maisha ya sasa ukilinganisha na hali ya tabia nchi
ilivyo pamoja na vyakula ambavyo vinaliwa kwa kipindi hichi.
Alisema kuwa kutokana na tatizo hilo kuonekana hivyo kampuni ya Phide entertaiment wameamua
kuandaa kuandaa maadhimisho haya kwa kuwapa fursa wanawake kujitokeza kupima
afya zao bure ambapo alisema tukio zima
litafanyika katika viwanja vya kumbukumbu ya Sheikh Amri Abeid kwa muda wa siku saba ambapo alisema kuwa maadhimisho haya yataanza
rasmi March 2 hadi March nane.
" tamasha hili kubwa linawapa fursa
wanawake kuweza kupima Afya yako
bure na magonjwa ambayo yatapimwa katika wiki hii ni pamoja na Moyo, Kisukari,
Macho, na figo hivyo napenda kuwasihi wanawake wenzangu wote wajitokeze kwa
wingi waje wapime afya zao na wajijue
vizuri "alisema Phide
Aidha alisema kuwa mbali
na kupima afya pia wiki hiyo itatumika kwa ajili ya kuwapa wanawake
ushauri juu ya kupima afya zao mara kwa mara
ambapo watawapa elimu ya kutosha .
"unajua kipindi hichi wanawake wamekuwa wanapata
magonjwa ya haina mbalimbali na wingine wamekuwa wanapuuzia kwenda hospitali
kupima afya zao mara kwa mara hivyo tamasha hili la wiki nzima litatumika
kuwaelimisha wanawake faida za kupima afya zao mara kwa mara"alisema Phide
Alimalizia kwa kuwataka wanawake wote kutopuuzia wiki
hiii kwani ni muhimu sana kwa kujotokeza kupima afya zao na wajue mfumo mzima
wa miiili yao ilivyo pamoja na kupata ushauri kutoka kwa wataalamu wa afya .
Post a Comment