CURRENT NEWS

Friday, March 10, 2017

MBUNGE WA VMAYSHAROSE MATTEMBE AENDELEZA HARAKATI ZA KUWAHUDUMIA WANANCHIMBUNGE wa Viti Maaalumu Mkoa wa Singida, Aysharose Mattembe,
anaendelea na harakati zake za kuwahudumia wananchi wa mkoa wake,
ambapo kwa sasa ametoa msaada wa vitanda 10 vya kujifungulia ili
kuhakikisha wajawazito wanajifungua salama. Amekabidhi msaada wake huo
kwa Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy
Mwalimu, ambaye alikuwa mgeni rasmi kwenye maadhimisho ya Siku ya
Wanawake Duniani mkoani kwetu Singida. Vitanda hivyo, tayari
vimekabidhiwa kwa Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa, Dk.
Ramadhan Mabala.

Pia, amesema anatambua changamoto nyingi zinazoikabili hospitali hiyo
katika kuwahudumia wananchi hususan wanawake wa Singida, hivyo
ataendelea kutumia uwezo wangu niliojaliwa na Mwenyezi Mungu katika
kuwahudumia.
 
Copyright © 2014 Mkono Wangu Production Designed by EvMak Tanzania