CURRENT NEWS

Wednesday, March 1, 2017

MCHENGERWA:WANANCHI WETU WANA IMANI KUBWA NA SERIKALI


Mbunge wa Rufuji Mohamed Mchengerwa akiwa na wanafunzi wa shule ya msingi iliyopewa jina na Mbunge huyo.
Mbunge wa Rufuji Mohamed Mchengerwa wa kushoto akiwa na Mwenyekiti wa Jumihiya ya Wazazi Wilaya ya Rufuji Ndg.Kaswakala Mbonde.  
 
Mbunge wa Rufiji, Mohamed Mchengerwa, (CCM) ameiomba serikali kuwaangalia kwa jicho la pekee wananchi wa pembezoni ambao wanapata tabu katika kupata huduma za kijamii ikiwemo suala la ukosefu wa maji.
Mchengerwa aliyasema hayo alipokuwa katika kijiji cha Miangalaya Mpakani ikiwa ni sehemu za ziara yake katika jimbo hilo baada kusikia kero kubwa ya maji kwani wananchi wanatembea zaidi ya kilomita 12 kutafuta Maji.
"Wananchi wetu wana imani kubwa na serikali pamoja na chama chetu lakini wapo nyuma katika maendeleo huduma nyingi muhimu hakuna na hili la maji ndio tatizo kubwa, naiomba serikali iwaangalie kwa jicho la pekee   kuipunguza kero ya maji na changamoto zingine kama za elimu,afya na barabara "alisema Mchengerwa
Alisema amehitahidi kuzungumza nje ya ndani ya bunge kuhusiana na umasikini unaowakabili wananchi wa jimbo lake lengo likiwa ni  kuirudisha Rufiji katika ramani kwani ilisahaulika ndio maana changamoto nyingi hazijapatiwa ufumbuzi.
"Nashukuru wananchi wangu mmeanza wenyewe jitihada za kujenga madarasa  naahidi kutoa mifuko 50 simenti pamoja na bati ili kukarabati shule hii ambayo mmeipa jina la Mchengerwa nitakuwa mlezi wenu "
Awali Mshamu Muba ambaye ni mkazi wa kijiji hicho  alieleza kuwa changamoto ya maji inawaumiza kwani wanaume wengi wanalea watoto ambao sio wa kwao kutokana  na wanawake zao kubakwa na kupewa mimba wakiwa wanatafuta maji umbali wa kilomita 12 kutoka majumbani.
 
Copyright © 2014 Mkono Wangu Production Designed by EvMak Tanzania