CURRENT NEWS

Friday, March 24, 2017

MEXICO:WANA HABARI WATATU WAUAWA MWEZI HUU

Muandishi wa habari nchini Mexico ameuawa kwa kupigwa risasi katika jimbo la Chihuahua, yeye ni mwana habari wa tatu kuuawa nchini humo mwezi huu.
Mirosalva Breach alipigwa risasi akiwa ndani ya gari lake nje ya makazi yake mjini Chihuahua.
Mmoja wa watoto wake ambaye alikuwa naye ndani ya gari, hakujeruhiwa.
Watu wenye silaha waliacha ujumbe uliosema '' kwa kuwa na mdomo mrefu''.
Bi Breach aliripoti kuhusu masuala ya uhalifu, biashara ya dawa za kulevya na rushwa katika gazeti la kitaifa, mjini humo La Jordana na Notre de Juarez.
Kamati inayotetea waandishi wa Habari imesema wanahabari 38 wameuawa nchini Mexico tangu 1992.
 
Copyright © 2014 Mkono Wangu Production Designed by EvMak Tanzania