CURRENT NEWS

Wednesday, March 1, 2017

MWANAMKE ACHOMWA AKIWA HAI KATIKA TAMBIKO NICARAGUA

Mume wa mwanamke aliyechomwa Vilma Trujillo aliagizwa kuchukua mwili wa mumewe katika chumba cha kuhifadhi maiti.
Mwanamke mmoja anayeishi katika eneo la mashambani nchini Nicaragua amefariki wiki moja baada ya kufungwa na kamba na kurushwa motoni katika tambiko la kufukuza mapepo.
Watu wa familia yake wameviambia vyombo vya habari kwamba Vilma Trujillo alishambuliwa na watu wanne wakiongozwa na mtu aliyesema kuwa ni muhubiri.
Juan Rocha alikana kumchoma bi Trujillo, akisema kuwa mapepo wabaya walimchukua na kumrusha motoni.
Mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 25 alipatikana na ndugu zake saa kadhaa baadaye akiwa na majeraha ya moto.
Maafisa wa polisi walimkatama bwana Rocha na watu fulani waliodaiwa kuhusika na uovu huo.
Mumewe mwathiriwa Reynaldo Perlata Rodriguez alisema kuwa mkewe alichukuliwa na kupelekwa kanisani wiki iliopita wakati wafuasi wa kanisa hilo walipodai kwamba ana mapepo baada ya kujaribu kuwashambulia watu kwa panga, kulingana na chombo cha habari cha AP.
''Hatuwezi kuwasamehe kwa kile walichotufanyia,alinukuliwa akisema.Walimuua mke wangu ,mama ya watoto wangu wawili sasa nitawaambia nini''?
Pablo Cuevas, msemaji wa tume ya haki za kibinaadamu nchini Nicaragua ametoa wito kwa serikali kudhibiti madhehebu ya kidini nchini humo.
 
Copyright © 2014 Mkono Wangu Production Designed by EvMak Tanzania